CCM WANATENGENEZA VITAMBULISHO FEKI.
Na Musa Makongoro.
Baadhi ya watendaji wa kata na vijiji wanashirikiana na wagombea wa CCM, kutengeneza vitambulisho feki vya kupigia kura.
Nae mmoja wa wanafamilia wa mwalimu Kelani Hujulwa,shule ya Sekondari Ukonga, amekili kuona wanafunzi wakiandikishwa nyumbani kwa kaka yake,muda wa usiku.
''Kuna wanafunzi huandikwa hapa usiku majina na vitambulisho vyao na wakati mwingine naona pia polisi wapo hapa wanazunguka, na huwa wanatumia gari nyeusi kuingia hapa''.
Mwandishi wa habari hizi aliweka kambi katika maeneo ya nyumba hiyo iliyopo eneo la Banana, yenye geti la rangi myeusi na kushuhudia mchezo huo,ambao unahusisha polisi waliovalia sare ya jeshi la polisi na wanafunzi ambao wanaingia nyumbani hapo wakiwa katika gari nyeusi aina ya prado,yenye namba T 456 AZP. Katika kuweka kambi hapo mwandishi ameweza kubaini kwamba gari hiyo, huingiza wanafunzi angalau mara mbili, na zoezi hilo hufanywa haraka haraka.
Uchunguzi unaonyesha kwamba viongozi wa CCM, wanashirikina na baadhi ya walimu wakuu, kupata wapiga kura feki, baada ya kugundua mchezo wa kupitisha kura zilizopigwa utakuwa mgumu zaidi kila kona ya nchi.
Mkakati wa kuwatumia wanafunzi umelengwa angalau kupata wanafunzi ambao ni wapiga kura feki 150 kutoka kila shule.
Kura hizi ni kwa ajili ya nafasi ya urais katika eneo husika.
Mmoja wa walimu kutoka shule ya sekondari Jitegemee,jijini Dar Es Salaam, anabainisha kwamba, mchezo huo unaratibiwa na baadhi ya walimu wakuu wa shule na wagombea wa CCM.
"Kuna posho wakubwa wetu wamepewa na pia wameambiwa wakiokoe chama kwa kutoa angalau wanafunzi 150 wasaidie kuongeza kura".
Wanafunzi hao ni ambao watatengenezewa vitambulisho feki,na kwamba, siku ya kupiga kura wanaweza kupiga kura katika maeneo mawili tofauti kwenye vituo vya kupigia kura.