CCM Wanagawa Fedha Mbezi

1954tanu

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2013
Posts
1,038
Reaction score
487
CCM wanagawa fedha kwa vijana ili kuwarubuni wajiunge na chama hicho na kuwashawishi wawaunge mkono kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa Mbezi Makabe.Harakati na mipango yao dhalimu wameanza kuifanya kitambo. Waliitisha mkutano wa dharula wiki moja iliyopita,mkutano ulidoda. Jana wakasambaza ujumbe kwa vijana kwamba wakutane jioni kwa mjumbe na kada wa Chadema kamanda Rama,almaarufu Ba'Dula.Walisema kada huyo anagawa fedha za Chadema.Vijana wakamfuata ili kuhoji kulikoni Chadema kugawa fedha! Sio utamaduni wa Chadema kufanya mambo ya kifirauni! Vijana wakiwa hapo kwa Ba'Dula wakaambiwa mwenyewe hayupo na wala hajui jambo hilo.

Ndipo mara wakaona gari la kada wa CCM ndg Sharifu linawasili hapo.Akatelemka ndg yake Ba'Dula. Vijana walipoona hivyo wakatawanyika.Baadaye,ilikuja julikana kwamba CCM wamekuwa wakigawa fedha kwa vijana tangu wiki iliyopita ili kuwavuta vijana wajiunge na kwenda kwenye mikutano ya chama chao.Mbinu hizo zimekwama.Kwa hiyo,wakaona watumie mbinu ya kuwaita vijana kwa kada wa Chadema kwamba ingerahisisha kuwapata vijana. Hilo limekwama maana Ba'Dula aliwajulisha vijana kwamba hakuwepo nyumbani muda ule na wala hakujua kinachoendelea akawataka vijana kutawanyika wasijihusishe na uzandiki huo wa kifisadi.Hali kwa jumla ni mbaya sana kwa CCM katika eneo la Mbezi Makabe. Vijana wengi wameikataa CCM.

Katika uchaguzi mkuu wa 2010 mgombea udiwani kwa tiketi ya CCM aliambulia kura 30 kati ya kura elfu kadha za mgombea udiwani wa Chadema kwa kura zilizopigwa katika kituo cha Shule ya Msingi Makabe.UKAWA huko Msumi.Wakati huo huo, katika eneo la Msumi CCM wamewafuata wafuasi wa CUF wakiwashawishi kwa fedha na kwa ahadi nyingi, huku wakitumia sera zao za ukanda na udini kwamba wasikubali Chadema kusimamisha mgombea kwa kiti cha mwenyekiti wa mtaa wa Msumi. Wanatumia mbinu hizo ili kuwagawa wananchi katika uchaguzi ujao.Njama hizi zimejulikana kwa sasa viongozi wa CUF na Chadema wanalifuatilia jambo hili kwa ukaribu.

Huko Msumi hali ya CCM nako ni tete, CUF na Chadema ni vyama vinavyokubalika zaidi eneo hilo.
 
Sio huko tu hata Mbezi Beach wanapita wanahonga 3,000/= kwa vijana na kina mama. Hata jana wameleta polisi kukamata vijana wa CDM wanaokaa katika pagala moja wakidai kuna wizi umetokea kwa hiyo wanawachukua kwa upelelezi.
Nawaasa vijana wasikubali kurubuniwa kwa kuhongwa pesa! Maana ukishachukua mgao wakikuona unaeneza sera za CDM ni shida.
Tujiandae kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura na twend kupiga kura tarehe 14.12.2014. Kitaeleweka tu.
 
Muondoe mkoloni mweusi CCM, ili uondoe umaskini...
 
CCM wanagawa fedha kwa vijana ilikuwarubuni wajiunge na chama hicho na kuwashawishi wawaunge mkono kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa Mbezi Makabe huku wakitumia jina la Chadema.

Harakati na mipango yao dhalimu wameanza kuifanya kitambo. Waliitisha mkutano wa dharula wiki moja iliyopita,mkutano ulidoda mkutano ulikuwa ufanyike katika ukumbi wa Bar ya Mwendi.

Jana wakasambaza ujumbe kwa vijana kwamba wakutane jioni kwa mjumbe na kada wa Chadema kamanda Rama, al-maarufu Ba'Dula.Walisema kada huyo anagawa fedha za Chadema.Vijana wakamfuata ili kuhoji kulikoni Chadema kugawa fedha! Sio utamaduni wa Chadema kufanya mambo ya kifirauni! Vijana wakiwa hapo kwa Ba'Dula wakaambiwa mwenyewe hayupo na wala hajui jambo hilo. Ndipo mara wakaona gari la kada wa CCM ambaye ni mmoja wa wanao wania kugombea nafasi ya mwenyekiti wa mtaa wa Makabe kupitia CCM, linawasili hapo.Akatelemka ndg yake Ba'Dula. Vijana walipoona hivyo wakatawanyika.

Baadaye,ilikuja julikana kwamba CCM wamekuwa wakigawa fedha kwa vijana tangu wiki iliyopita ili kuwavuta vijana wajiunge na kwenda kwenye mikutano ya chama chao.Mbinu hizo zimekwama.Kwa hiyo,wakaona watumie mbinu ya kuwaita vijana kwa kada wa Chadema kwamba ingerahisisha kuwapata vijana. Hilo limekwama maana Ba'Dula aliwajulisha vijana kwamba hakuwepo nyumbani muda ule na wala hakujua kinachoendelea akawataka vijana kutawanyika wasijihusishe na uzandiki huo wa kifisadi.

Hali kwa jumla ni mbaya sana kwa CCM katika eneo la Mbezi Makabe. Vijana wengi wameikataa CCM. Katika uchaguzi mkuu wa 2010 mgombea udiwani kwa tiketi ya CCM aliambulia kura 30 kati ya kura elfu kadha za mgombea udiwani wa Chadema kwa kura zilizopigwa katika kituo cha Shule ya Msingi Makabe.

UKAWA huko Msumi.

Wakati huo huo, katika eneo la Msumi CCM wamewafuata wafuasi wa CUF ambao wanania ya kugombea kiti cha mwenyekiti wa mtaa wa Msumi, wakiwashawishi kwa fedha na kwa ahadi nyingi, huku wakitumia sera zao za ukanda na udini kwamba wasikubali Chadema kusimamisha mgombea kwa kiti cha mwenyekiti wa mtaa wa Msumi.

Wanatumia mbinu hizo ili kuwagawa wananchi katika uchaguzi ujao.Njama hizi zimejulikana kwa sasa viongozi wa CUF na Chadema wanalifuatilia jambo hili kwa ukaribu. Huko Msumi hali ya CCM nako ni tete, CUF na Chadema ni vyama vinavyokubalika zaidi eneo hilo
 
SASA BUKU 3 / AU 3.000/= AU KOFIA AU KHANGA vitakusaidia nini? BAADA YA KUPONZEKA NA VITU HIVYO #TAFAKARI ! TUSIRUBUNIWE
 
Umaskini ni laana uliyozaliwanayo haikusababishwa na CCM

Hujitambui wewe, we unadhani kila mpinga CCM ni mla vumbi kama wewe huko Kimbangulile...
 
kweli mkuu mimi jana walinipa milioni hamsini na rafiki yangu wakampa milioni kumi na tano.
 
juzi walikuwa boko basihaya, masikini kumbe uchaguzi wa hii nchi ukiwa fair hawatapona hawa fisi maji.
 
Umaskini ni laana uliyozaliwanayo haikusababishwa na CCM

We ndo pimbi kabisa ccm wanawapora mpaka wazee vijijini vipesa vyao eti maabara wewe unachekelea
ccm wanaiba madini yetu wanyama wetu pesa za umma wewe huoni au kipofu?
 
Nyie chukueni hizo pesa zao mkawape watoto iwe pesa ya kula mihogo wakati wa mchana.
 
Umaskini ni laana uliyozaliwanayo haikusababishwa na CCM

Inatoka moyoni kweli!!!!!Nchi zote zilizoendelea ni kwasababu zimekuwa na siasa safi,sera nzuri,uongozi bora na uwajibikaji
 
Mkanichukulie NA Mimi jaman nakuja tusipozipata kipindhiki cha uchaguzi tutazipata wapi tena
 
Kula CCM kura upinzani principle should be applied.Over
 
Ccm haina upuuzi huo
cc
mleta mada
Ndugu acha kupinga kila jambo.Tunayoyaandika tumeyashudia.

Au huku mwelewa mh.Kinana aliposema CCM imejaa rushwa? Ok.Huyo huku mwelewa, je mzee Butiku naye hujamwelewa. Ok,,na Mwl.Nyerere aliposema CCM ina nuka rushwa pia naye hujamwelewa.

MIT.25:25 Mtu anayesemaa mtu mwovu ana haki, jamii itamchukia taifa litamlaani..

UPO HAPO!
 
Umetumia misamiati migumu sana kwa akili ya vibaka wa ccm kukuelewa. Utashangaa wankuja hapa na mapovu kumwaga pumba bila kugusa hoja ulizozisema hata punje. Mingoi; njoo hapa umjibu kamagetac;


Inatoka moyoni kweli!!!!!Nchi zote zilizoendelea ni kwasababu zimekuwa na siasa safi,sera nzuri,uongozi bora na uwajibikaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…