CCM wamshambulia mdhamini CHADEMA

CCM wamshambulia mdhamini CHADEMA

ndiyomkuusana

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
668
Reaction score
426
hasanali.jpg

MJUMBE wa Bodi ya Wadhamini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Muslim Hassanali, amedai kushambuliwa na Katibu Kata wa Kisutu kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Sauda Addey, baada ya mjumbe huyo kukataa kubandikwa kipeperushi cha wagombea wa nafasi ya uenyekiti wa serikali za mitaa kupitia CCM mbele ya eneo lake la biashara.Hassanal, anadai tukio hilo lilitokea Jumamosi saa tano asubuhi, baada ya wafuasi wa CCM kubandika kipeperushi chao katika eneo lake la biashara lililopo mtaa wa Mali Kisutu jijini Dar es Salaam.
Kushambuliwa kwa Hassanal, kumekuja ikiwa ni siku chache zimepita huku baadhi ya wafuasi wa vyama vya siasa katika maeneo mbalimbali nchini wakiwa wameshashambuliana na wengine kupoteza maisha.
Akizungumzia namna alivyoshambuliwa, Hassanal alisema baada ya kufika ofisini kwake, alikuta kipeperushi hicho na alipouliza watu aliowakuta wakamuambia kuwa makarataisi hayo yamewekwa usiku na kwamba hawamjui aliyeweka.
“Kisheria lile ni eneo langu ninalolimiliki kibiashara, hivyo yeyote anayetaka kulitumia ni lazima aonane na mimi nimpe ruhusa ama la, sasa hawa CCM wamekuja kuweka pasipo ridhaa yangu na mimi siipendi CCM, nikiona hata rangi zao nasikia kichefu chefu nikaona ngoja niziondoe,” alisema Hassanal na kuongeza;
Unajua ile ni sehemu ya biashara wanafika watu wa kila itikadi, sasa kubandika picha kama zile zinaweza kuvuruga biashara zangu, isitoshe kwa kulitambua hilo ndio maana nimeshindwa hata kubandika picha za wagombea wa CHADEMA ambacho ni chama changu.
Alidai kuwa, baada ya kuyaondoa matangazo hayo viongozi wa Kata hiyo wa CCM wakiambatana na wafuasi wao, walimvamia na kumfanyia vurugu zilizosababisha uharibifu wa miwani yake ya macho, vifaa, nyaraka na upotevu wa baadhi ya vitu.
Alisema kutokana na fujo hizo, alifika kituo cha Polisi Kisutu, ambako wakamueleza hawana mamlaka ya kushughulikia kesi za kisiasa, hivyo alifikishe suala hilo kituo kikuu cha kati.
Hassanali, alisema baada ya kushauriwa hivyo, aliamua kwenda kituo hicho lakini cha kusikitisha hakuweza kupata ushirikiano wa kutosha na alitakiwa kurudi kituoni hapo Jumatatu, ambako alifanya hivyo.
“Leo kama mnavyoniona hapa bado nasumbuliwa, nataka kufungua jalada lakini bado wahusika wanazunguka tu kwa kunieleza kuwa msimamizi wa shauri langu hajafika, hata hivyo niliweza kuhojiwa na kuandika maelezo yangu,” alisema.
Wakili wa Hasanali, Fredrick Kihwelo, alikiri mteja wake kufanyiwa vurugu na kwamba baada ya kufika polisi, waliandika maelezo na kuambiwa uchunguzi unaendelea.
“Pamoja na kukwama siku ya Jumamosi, leo tumekuja tena, tangu asubuhi tuko hapa na hatimaye tumefungua kesi ya jinai, kimsingi suala hili litakuwa kwenye uchunguzi baada ya hapo litapelekwa kwa DPP ambaye ndio ataamua kama litapelekwa mahakamani,” alisema wakili huyo.
Kwa upande wake, Sauda alisema zoezi la kubandika picha za wagombea limefanyika Jiji zima kisheria tangu miaka ya nyuma na hakutegemea katika eneo hilo kama angekuwepo mtanzania mwenye asili ya Asia asiwe mfuasi wa CCM.
“Sisi hatukujua kama pale kuna mtu wa CHADEMA tena Muhindi, kama tungejua tusingebandika, kwani kwa zaidi ya miaka 25 tumekuwa tukibandika,” alisema Sauda.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Mary Nzuki, alisema suala hilo bado liko kwa mkuu wa kituo kwa ajili ya uchunguzi na mara litakapokamilika litafikishwa kwake kwa hatua zaidi.
 
Hoja yako iko wapi unapenda wazungu kama mzee slaa anavyowapenda wazungu sijui wanawapa nini.
 
Hapo atazungushwa mpaka basi, kisa yuko CHADEMA. Nchi itavurugika kwa vyombo vya dola kutotenda haki wa kuangalia itikadi ya mtu.
Nchi inamiko yake haiwezi kuvurugwa na ujinga wa chadema kama unavyodhani.
 
Vyombo vyetu vya dola burudani sana. Nikukumbuka like tukio la OCD Kula makofi ya mgombea wa CCM, nacheka sana.
 
sisi wapinzani tutawashambulia hao ccm kwenye uchaguzi mkuu kama tulivyofanya siku chache zilizopita kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa
 
Hilo lichama limejigeuza kutoka Chama cha siasa na badala yake kimekuwa kikijishughulisha na mambo mengineyo.

Ndiyo maana kirefu cha chama hicho kimegeuka na kuwa Chama cha Mafisadi, Chama cha Magamba, Chama cha Matunguri, Chama cha Maescrow, na sasa kimekuwa pia Chama cha Mabondia!
 
Hoja yako iko wapi unapenda wazungu kama mzee slaa anavyowapenda wazungu sijui wanawapa nini.

Hapana umekosea! Sema hivi, "UNAPENDA WAZUNGU/WACHINA KAMA PROFESELI KIKWETE! MAANA HAISHI KWENDA KUPIGANAO PICHA KWA MWEZI MARA 3!".
 
Atakuwa na undugu na lile punga Mustafa Hassanali.
 
View attachment 212649

MJUMBE wa Bodi ya Wadhamini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Muslim Hassanali, amedai kushambuliwa na Katibu Kata wa Kisutu kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Sauda Addey, baada ya mjumbe huyo kukataa kubandikwa kipeperushi cha wagombea wa nafasi ya uenyekiti wa serikali za mitaa kupitia CCM mbele ya eneo lake la biashara.Hassanal, anadai tukio hilo lilitokea Jumamosi saa tano asubuhi, baada ya wafuasi wa CCM kubandika kipeperushi chao katika eneo lake la biashara lililopo mtaa wa Mali Kisutu jijini Dar es Salaam.
Kushambuliwa kwa Hassanal, kumekuja ikiwa ni siku chache zimepita huku baadhi ya wafuasi wa vyama vya siasa katika maeneo mbalimbali nchini wakiwa wameshashambuliana na wengine kupoteza maisha.
Akizungumzia namna alivyoshambuliwa, Hassanal alisema baada ya kufika ofisini kwake, alikuta kipeperushi hicho na alipouliza watu aliowakuta wakamuambia kuwa makarataisi hayo yamewekwa usiku na kwamba hawamjui aliyeweka.
“Kisheria lile ni eneo langu ninalolimiliki kibiashara, hivyo yeyote anayetaka kulitumia ni lazima aonane na mimi nimpe ruhusa ama la, sasa hawa CCM wamekuja kuweka pasipo ridhaa yangu na mimi siipendi CCM, nikiona hata rangi zao nasikia kichefu chefu nikaona ngoja niziondoe,” alisema Hassanal na kuongeza;
Unajua ile ni sehemu ya biashara wanafika watu wa kila itikadi, sasa kubandika picha kama zile zinaweza kuvuruga biashara zangu, isitoshe kwa kulitambua hilo ndio maana nimeshindwa hata kubandika picha za wagombea wa CHADEMA ambacho ni chama changu.
Alidai kuwa, baada ya kuyaondoa matangazo hayo viongozi wa Kata hiyo wa CCM wakiambatana na wafuasi wao, walimvamia na kumfanyia vurugu zilizosababisha uharibifu wa miwani yake ya macho, vifaa, nyaraka na upotevu wa baadhi ya vitu.
Alisema kutokana na fujo hizo, alifika kituo cha Polisi Kisutu, ambako wakamueleza hawana mamlaka ya kushughulikia kesi za kisiasa, hivyo alifikishe suala hilo kituo kikuu cha kati.
Hassanali, alisema baada ya kushauriwa hivyo, aliamua kwenda kituo hicho lakini cha kusikitisha hakuweza kupata ushirikiano wa kutosha na alitakiwa kurudi kituoni hapo Jumatatu, ambako alifanya hivyo.
“Leo kama mnavyoniona hapa bado nasumbuliwa, nataka kufungua jalada lakini bado wahusika wanazunguka tu kwa kunieleza kuwa msimamizi wa shauri langu hajafika, hata hivyo niliweza kuhojiwa na kuandika maelezo yangu,” alisema.
Wakili wa Hasanali, Fredrick Kihwelo, alikiri mteja wake kufanyiwa vurugu na kwamba baada ya kufika polisi, waliandika maelezo na kuambiwa uchunguzi unaendelea.
“Pamoja na kukwama siku ya Jumamosi, leo tumekuja tena, tangu asubuhi tuko hapa na hatimaye tumefungua kesi ya jinai, kimsingi suala hili litakuwa kwenye uchunguzi baada ya hapo litapelekwa kwa DPP ambaye ndio ataamua kama litapelekwa mahakamani,” alisema wakili huyo.
Kwa upande wake, Sauda alisema zoezi la kubandika picha za wagombea limefanyika Jiji zima kisheria tangu miaka ya nyuma na hakutegemea katika eneo hilo kama angekuwepo mtanzania mwenye asili ya Asia asiwe mfuasi wa CCM.
“Sisi hatukujua kama pale kuna mtu wa CHADEMA tena Muhindi, kama tungejua tusingebandika, kwani kwa zaidi ya miaka 25 tumekuwa tukibandika,” alisema Sauda.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Mary Nzuki, alisema suala hilo bado liko kwa mkuu wa kituo kwa ajili ya uchunguzi na mara litakapokamilika litafikishwa kwake kwa hatua zaidi.

Nmecheka sana na kustaajabu! Yaani ukiwa Muhindi pale Kisutu lazima uwe CCM? Inashangaza sana!

Ukiwa huna chama kwa mfano je ni halali kubandikiwa picha za wagombea ambapo wewe mwenye eneo uko neutral, eti kisa tu kwamba Kisutu yote Wahindi ni CCM? Ni jambo la kustusha hasa majibu hayo ya muhusika wa CCM. Ifike wakati Watanzania wajiandae kisaikolojia, kwamba kwa kuruhusu mfumo wa vyama vingi basi tambua watu watakuwa huru kimitazamo na hiyo siyo dhambi ili mradi huvunji sheria za nchi!
 
Hapo atazungushwa mpaka basi, kisa yuko CHADEMA. Nchi itavurugika kwa vyombo vya dola kutotenda haki wa kuangalia itikadi ya mtu.

Nyumba sio yake ni mpangaji tu wa NHC ndio maana kapigwa na mtoto wa kike kwa kuwa ni farasi.
 
Huyu Hasanali mbona hafanani na Chadema

Huyo ni Chadema damudamu ndiye aliyekuwa mgombea Ubunge jimbo la Kigoma kusini tangu 2005 mpaka2010.Tatizo nyie Mi ccm mnafikiri eti Wahindi wote wanawapenda bila kujua kuna Wahindi Watanzania tena wazawa.Huyo jamaa ndiye aliyehujumiwa nayule kibaraka wenu Zitto akawa anamfanyia kampeni Kafulila
 
Hilo lichama limejigeuza kutoka Chama cha siasa na badala yake kimekuwa kikijishughulisha na mambo mengineyo.

Ndiyo maana kirefu cha chama hicho kimegeuka na kuwa Chama cha Mafisadi, Chama cha Magamba, Chama cha Matunguri, Chama cha Maescrow, na sasa kimekuwa pia Chama cha Mabondia!
chama cha mabusha au mate I
 
Vyombo vyetu vya dola burudani sana. Nikukumbuka like tukio la OCD Kula makofi ya mgombea wa CCM, nacheka sana.
haa haa mkuu umenikumbusha mbali, halafu Mtu mwenye cheo kama hicho anatandikwa makofi na mgombea wa chama tawala. Halafu hatua hazichukuliwi. Taifa hili tuna double standard sana katika maamuzi.
 
Back
Top Bottom