Mtini
JF-Expert Member
- Apr 28, 2011
- 1,491
- 2,355
Kama kawaida yangu naomba kudeclare interest mapema "SIFUNGAMANI NA CHAMA CHOCHOTE"
Katiba ya CCM ya mwaka 77 toleo la 2010 ibara ya 118 inasema,
Mwenyekiti wa CCM ndiye kiongozi mkuu na
ndiye msemaji mkuu wa CCM.
(1) Atachaguliwa na Mkutano Mkuu wa
CCM wa Taifa na atakuwa katika nafasi
hiyo ya uongozi kwa muda wa miaka
mitano, lakini anaweza kuchaguliwa
tena baada ya muda huo kumalizika.
Ibara ya 104 inasema,
(1) Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa
utakuwa na wajumbe wafuatao:-
(a) Mwenyekiti wa CCM.
(b) Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania
wanaotokana na CCM.
(c) Makamu wawili wa Mwenyekiti wa
CCM.
(d) Rais wa Zanzibar anayetokana na
CCM.
Tangu mwanzo katiba ya CCM ilitenganisha urais na uenyekiti na ikatoa haki kwa kila mwanachama kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi ya uenyekiti taifa. Katika ibara hizi hatuoni mahali Rais akitajwa kuwa ni lazima kushika nafasi ya uenyekiti. Katika hali ya kuminya democrasia chamani wakaingiza hii kitu inaitwa "UTAMADUNI" ambayo inakandamiza uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa. Nina maswali mawili kwa wanaccm
1. Utamaduni ni zaidi ya katiba?
2. Kama mmeshindwa kuheshimu katiba mliyojitungia wenyewe mtaheshimu katiba ya nchi?