Elections 2010 ccm wamesaidia sensa muhimu tanzania

realtz7

Senior Member
Oct 23, 2010
110
1
kwa matokeo ya mwka huu percent watayopata ccm dio exactly idadi ya wajinga wa tz, wasiojua kusoma, kuandika, na kuchambua mambo. ukitaka kuniprove sahihi just angalia maeneo ccm walioshinda uone maendeleo yake, raia wake, hao ndo wanaifanya tz iwe kumi bora ktk umaskini kwa miaka yote! tunawalisha na kuwafanyia kazi, wao wamebai kuwa wamachinga na kutembeza mboga mitaani! kuikomboa tz lazma kelimisha hii jamii kwanza, ila lindi mtwara, bagamoyo elimu hiyo kazi ipo!
 
Uko sahihi sana mkuu kwa kweli hali katika maeneo hayo ni mbaya na wananchi hawataki kubadilika kabisa. Aibu kwa watanzania na aibu kwa taifa zima
 
Jamani, si kila mtu ana haki ya kumchagua ampendaye? Ni nini maana ya demokrasia? Ni lini kuichagua CHADEMA au chama kingine cha upinzani imekuwa ni kipimo cha elimu ya Mtanzania?
Ingawa nimesikitishwa na matokeo ya upinzani katika maeneo hayo, sioni kama ni sawa kuwatukana au kuwakejeli watu walioamua kutumia haki yao kuichagua CCM.
Si ndiyo demokrasia tunayoipigania kila kukicha? Je tuseme nini juu ya wapinzani wa huko ambao hawakujitokeza kupiga kura?
Labda wapinzani tutumie fursa hii kuona ni maeneo gani ya kuongeza nguvu kwa kipindi hiki ili tujizatiti kwa uchaguzi ujao. Matusi hayatatusaidia, kwani yatatufanya tuonekane hatuna maana kama CCM wanaolala wakitegemea mbwembwe na kashfa wakati wa kampeni ili washinde.:israel:
 
Ili demokrasia ikamilike ni lazima wapiga kura kwanza wajue haki zao za msingi.Tanzania ya leo bado wananchi hawajapewa elimu ya uraia na elimu kwa ujumla ya kuweza kutambua uongozi dhalimu.Kwao wengi ili waone chama au serikali imeshindwa kazi,basi kipimo chao kikubwa ni hali ya amani na utulivu uliopo!Hata wapigiwe kelele namna gani kuhusu wao kunyonywa,kuonewa na kuibiwa rasilimali zao hawakuelewi kwa kuwa kipimo chao cha amani na utulivu bado wanaamini hakijatetereka!Kwanini?Ni kwakuwa hawajui na hawatambui nini wajibu wa viongozi wao pale wanapowapa madaraka.Kwa hiyo ucpinge kwamba wanaopigia kura ccm ama ni wajinga na/au wanamaslahi na huu udhalimu uliopo.Serikali ya ccm imeendelea kumnyima mwananchi elimu hii ili iendelee kumuibia na kufaidisha kikundi cha watu wachache.
 
Back
Top Bottom