CCM tunakosea wapi? Hii tabia ya kusomba watu kwenye malori kwenye mikutano ya hadhara mpaka lini? Mbona Chadema wanajaza nyomi bila kusomba watu?

mwananyaso

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
2,843
3,128
Katika jambo ambalo linanikera ni hili la kusomba watu kuhudhuria mikutano ya hadhara ya CCM,tatizo hili limekuwa common sana, mfano ni mkutano wa Chongolo mwanza hivi karibuni.Ifahamike pia Hamonize alisaidia kuokoa jahazi.

Nakumbuka enzi za hayati Magufuli akiwa ziarani mikoani njiani wanannchi walivutiwa nae sana,walipenda kumfatilia na kumsikiliza na walijenga imani na CCM.

Taarifa ya habari iliwavutia sana watanzania kumsikiliza hayati Magufuli.

Kwasasa inaonyesha CCM imechokwa gafla sana, Chadema inachanja mbuga kwa kasi sana,

Tatizo nini? Au ni wastaafu wasiotaka kustaafu, wamechokwa?
 
Wananchi walishaichoka ccm kitambo, ni mnalazimisha tu mambo.

Unajaribu kusema Magufuli alikuwa anajaza nyomi, lakini ndiye muasisi wa malori
Ila angalau Rais Magufuli aliirudisha imani ya ccm kwa wananchi

Kuthibitisha hilo akiwa njiani wananchi walijitokeza kwa wingi kuzungumza nae,pia ile style yake ya kutatua kero papo kwa hapo, ilijenga imani kwa wananchi.

Sasa huyu wa sasa Msafara wa magari yake ni mkubwa kuliko wahudhuriaji
 
This is politics, tumia chochote ujumbe wako na kusudi la ujumbe wako uwafikie wengi iwezekanavyo kwa gharama yeyote na lengo litimie kikamilifu.

Siasa ni kama Mchezo wa Ngumi ukizembea utachapwa mapema sana na huku ukilaumu aina ya ngumi ulopigwa 🤓
 
Wekamo na tupicha basi
Mafundi umeme
20230801_151854.jpg
 
Back
Top Bottom