Imekuwa kawaida sana kuchukua watu huku na kuwapeleka kule kunako mikutano yetu ya kampeni za kisiasa. Watu hawa hubebwa kwa kila aina ya usafiri: mabasi makubwa na madogo, malori, matrekta, power tiller na mwingineo. Huku tuki walipa malipo ya kuhudhuria kwao elfu tano tano, elfu mbili mbili, sare, kofia TShirt nakadhalika.
Watu awa hawa walihudhuria ama watahudhuria mkutano mwingine wa mgombea wa upinzani wakijihudhurisha wenyewe. Wanaenda kwa miguu yao tena pasipo kulipwa chochote kwa umbali ule ule tuliowabeba kwa magari.
Hawa watu wanatuonaje; wanatuchukuliaje?
Kwamba tumechanganyikiwa? Ama ghafla tu tumewapenda sana? ama watuonee huruma tumekosa watu? ama sisi ni mazuzu fulani hivi? ama tumekuwa mabuzi, tumejipeleka tuchunwe? ama sasa ndio tunaanza kuona umuhimu wao? ama sisi ni mabwege fulani hivi, kwa hiyo wanatugida?
Halafu jioni ama siku ifuatayo, wanajiona kwenye vyombo vya habari "mafuriko" makubwa wamkubali mgombea wetu. Na huku wangali wanajua jinsi walivyofurikishwa,hawa hawakufurika eti! Wanatuonaje fikrani mwao? Wanamwonaje mgombea wetu anavyo jishebedua mbele ya watu waliofurikishwa?
Tusaidiane. Isije ikawa ni "Tumgidie -----" ya marehemu John Rutahayasingwa kwenye yale magazeti ya Mzalendo Enzi zile..