Ellyson
JF-Expert Member
- Nov 13, 2010
- 1,714
- 405
Mwaka 1995 Mwalimu Nyerere alimshika mkono Benjamini Mkapa akituomba tumchague kwa kuwa ni msafi na hana doa. Alitembea nchi nzima akimnadi kama mgombea mwenye uwezo wa kututoa kwenye dimbwi alimotutumbukiza mtangulizi wake Ali Hassan Mwinyi. Haikupita miaka miwili Mwalimu huyo huyo alikuwa jukwaani tena akilaani vitendo vya Mkapa kuuza mali za wananchi kama hana akili nzuri. NI MFUMO ULIOMBADILISHA MKAPA. Mwaka 2005 Jakaya Kikwete alinadiwa kwa watanzania kama chaguo la Mungu, kama mgombea ambaye Taifa lilikuwa linamsubiria kurudisha Tumaini lililopotea. Alihaidi kuingia kwa Kasi Mpya, Ari Mpya Nguvu Mpya na Maisha Bora kwa kila mtanzania.
Aliahidi kwenye Urais hatakuwa na mbwembwe. Haikuchukua miaka miwili kashfa baada ya kashfa zikaanza kuiandama Serikali ya Rais Kikwete hadi akashindwa kutulia nyumbani na kugeuza anga ndio ofisi yake. Leo anakwenda kupumzika huku akisema "hajui kwanini sisi ni maskini" NI MFUMO ULIOMBADILISHA KIKWETE. Mwaka huu 2015 tunaombwa tena na chama kile kile, watu wale wale wenye fikra na mawazo yale yale na utawala ule ule tumchague John Pombe Magufuli kwa sifa za Utendaji, ukakamavu(kupiga pushup jukwaani), hapa kazi tu. Safari hii tunaletewa ambaye kwa usafi na uadilifu hamfikii Mkapa, kwa mbwembwe hamfikii Kikwete na bingwa wa kukurupuka tunaombwa tumpe kura alinasue Taifa.
Ameshaanza kwa kushangaa na hajui kwanini waliomtangulia hawakufanikiwa. KAMA HUJUI HUO NDIO MFUMO...silazimishi wala sihitaji kulazimisha maana kila mtu ana uhuru wa kuchagua apapendapo,ila kwa wachache wasio mashabiki uchwara na wanamabadiliko nawasihi ifikapo october 25 tusifanye makosa..Mungu ibariki UKAWA(CHADEMA),Mungu mbariki EL mtu pekee awezae kuokoa jahazi lilozama japo anaonekana dhaifu kati ya wengi wajionao na NGUVU.