Mwanzo ni ukweli kwamba umri wa kati wa Tanzania ni miaka 17.8. Kwa namna hii Matanzania wa kati kwa sasa ni mtoto! ambaye hawezi hata kupiga kura. Zaidi ya asilimia 64 hivyo ya Watanzania wapo chini ya miaka 24. Hivyo basi wapiga kura wa miaka kumi ijayo asilimia zaidi ya 80% watakuwa wapya na kizazi kipya. Kwasababu hii upinzania sio swala la kupuuzia. Kizazi hiki cha sasa hakuna siri hata kama udikteta unaongezeka. Kitu kimoja ambacho CCM inatakiwa kufanya ni lazima waweke mikakati ya maendeleo ya vijana sio kwa kazi tu bali elimu ya kisasa. Ushindani wa miaka ijayo hautatoka Tanzania bali vijana wa nchi nyingine maana itafikia wakati mchora ramani yako ya nyumba hayupo Tanzania, mtengeneza computer yako hayupo Tanzania, Accountant ya makampuni hawapo Tanzania... kazi zote zenye technologia huwezi kuzizuia tena. Kwa ufupi adui kubwa wa CCM sio Chadema bali ni watu kubadilika hivyo kama CCM inataka kuendelea kuwa na support ni lazima wabadilishe mifumo hasa ya kielimu ili ziende na ushindani wa sasa wa kimataifa. Vilevile bila kutoa haki vizuri watu watahamia upinzania ....