CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimeogopa kuzungumzia suala la Katiba mpya kikisema kuwa kinangoja kupata msimamo huo toka kwa Rais Jakaya Kikwete. Akizungumza na Tanzania Daima jana, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, alisema wao kama chama hawawezi kuzungumzia suala hilo na kwamba msimamo utakaotolewa na mwenyekiti wao ambaye ni Rais ndio utakaokuwa wa chama.
'Mimi nasema wahariri si walikaa na Waziri Mkuu'¦akasemaje...akasema atamshauri Rais sasa ukinitaka mimi niseme, nasema Katiba ipo lakini ninataka iwe na maudhui gani?