CCM ni ya nani?

Chama dola

CCM ni mfumo, inatawala, kuongoza na kuelekeza kila kitu katika taifa, mpaka maisha yako, uongee nini uishi vp upataje pesa nk, wanamiliki mpaka uchumi wako wakiamua kukufilisi au kukupoteza ni sekunde tu.

Lakini chini ya jua kila lenye mwanzo lina mwisho, tena mwisho wao utakuwa mbaya sana, chukua hiyo.
 
Ccm haina mwenyewe ila baadhi yetu kwa ulimbukeni wa madaraka hufikiria tunaimiliki.
 
Ccm haina mwenyewe ila baadhi yetu kwa ulimbukeni wa madaraka hufikiria tunaimiliki.
Nakubaliana na wewe, inavyoonekana kwenye mchakato wa kuiua TAA na kuunda TANU na kuia TANU kuunda CCM kulikuwa na nia ovu ya kuwany ang'anya wenye chama halisi na Kaia pa wasiojulikanna. Chama sasa hivi kimegeuka nyangumi kuvusha makundi ya watu fulani kwenda Ikulu kwa maslahi yao. Kwa mbaaaali at the end of the tunnel kwakutumia kiona mbali unaweza kuiona mikono ya dini fulani na nchi kubwa za kizungu kwenye umiliki wa sasa. Atakaempanda na kuvushwa salama na nyangumi huyo lazima ajibu swali LA "utaifanyia nini dini hiyo na nchi hizo" kama utababaika kwenye kulijibu swali hilo ama humpandi nyangumi huyo kabisa au ukifanikiwa kumpanda na kufika utapata misukosuko mingi.

Sharti kuu LA mwisho unalopewa na wamiliki ni kuhakikisha kuwa chama hakii mikononi mwako, ufanya ufanyavyo kisifie kwako iwe mvua liwe jua.

Taja sababu angalau 3 tu za kuia TAA na kuunda TANU.
 
Kama Mwalimu Nyerere mwanzilishi wa CCM alisema CCM si mali yake wala haijamzaa Nape ni nani anayedai CCM inawenyewe? Nape ahamini kwenye Taasisi inaonekana anawatu pale anawategemea.
 
Kama Mwalimu Nyerere mwanzilishi wa CCM alisema CCM si mali yake wala haijamzaa Nape ni nani anayedai CCM inawenyewe? Nape ahamini kwenye Taasisi inaonekana anawatu pale anawategemea.
Nape sio mwenyewe, ni mnufaika tu. Angekuwa sehemu ya wenyewe asingetolewa bastola hadharani auawe. Wenye ccm wanaweza kumshughulia yeyote yule mwenye mdomomdomo na kuzuia maslahi yao bila kujali alishawahi kuwa nani na ni nani kwenye nchi hii. Hata Mwenyekiti wa chama lazima asitofautiane nao kwenye maslahi yao. Jamani hili ni zimwi linalotafuna kila MTU na kila kitu. No one is safe hata wanaojiita wanaCCM kindakindaki. Mwenye remote control ya dubwasha hili hayuko Tanzania na sio mtanzania pengine.

Hata tunaoimba hiyena iyena kwa miaka 60 tuko gizani kwenye vijumba vya udongo na manyasi bila maji ya kunywa wala barabara, na kijembe cha mkono shambani tumepigika huku madini, Mbao, samaki, wanyama pori na rasilimali zetu zikisombwa kwa matani kwa matani kwenda kwa wenye chama.

Amkeni amkeni amkeni amkeni kwenye usingizi.
 
Kama Mwalimu Nyerere mwanzilishi wa CCM alisema CCM si mali yake wala haijamzaa Nape ni nani anayedai CCM inawenyewe? Nape ahamini kwenye Taasisi inaonekana anawatu pale anawategemea.
Waafrika wooote lazima tukubaliane kuwa wakoloni hawakuondoka Africa kwa kupenda, lakini hawakuondoka kiboyaboya pia. Walijipanga kuondoka na walifanya maandalizi ya kuondoka. Kuwasomesha akina Mwl Nyerere huko ulaya ilikuwa sehemu ya maandalizi hayo.

Mwl nyerere aliporudi tu kutoka masomoni ulaya alikimbilia kukiua chama cha TAA na kuunda TANU badala ya kukiongezea nguvu TAA ambayo tayari ilikuwepo. Baadae akakimbilia muungano na Zanzibar na baadae akakimbilia kuunda CCM na baadae akakimbilia chama kushika hatamu. Hebu jiulize ni kwanini Mwl nyerere, Jomo Kenyatta, Kamuzu Banda, na Moboutu walinusurika kuawa wakati marais wengine wakipukutishwa? nani alikuwa akiwalinda, kwa faida gani na kwa huruma gani? Je, ni kweli mfumo wetu wa kumlinda ulikuwa mzuri sana kuliko ya nchi za kikoloni?
 
Ukisoma gazeti la Mwananchi la leo tarehe 23/12/2021, ukurasa wa tatu, kuna baadhi ya WENYE CCM wameorodheshwa. Ni untouchables. Ukitaka kuwajua zaidi, wametajwa kwenye ripoti aliyoandaa Bashiru miaka ile juu ya mali za CCM, jiulize kwa nini JPM na ubabe wake wote hakusoma hadharani ile ripoti.
 
Ccm haina mwenyewe ila baadhi yetu kwa ulimbukeni wa madaraka hufikiria tunaimiliki.
Wale waliotumia akili, nguvu na rasilimali zao kuanzisha TAA na Afro-Shiraz zilizokuja kuzaa TANU na CCM wako wapi? watoto na wajukuu wao wamefichwa wapi? Kuna kila dalili kuwa kulikuwa na mpango mahususi ulioratibiwa na watu makin wa ndani na nje kuwapora TAA na Afro-Shiraz waazilishi wake. Kwenye hili waliopata hasara kubwa zaidi ni waanzilishi wa TAA kuliko wenzao wenzao wa Afro-Shiraz.
 

bado uwafahamu na leo wengine wanaendelea kupata teuzi na keki ya nchi na mpaka vitukuu vitakula teuzi
 
CCM ni 3+3+13 inaleta 19 sawa sawa na 1 (mmiliki wake alishakufa hivyo laana ya kukiita ni chama cha mapinduzi karma inawaangamiza kila mwenye kupata mwanya wa kumpindua mwingine na kumiliki kwa muda anafanya hivyo akizubaa anapinduliwa kinaenda kwenye mikono mingine ispokuwa tu uwe ni mbobezi wa fitina, majungu, unafiki, uongo, uzushi, mshirika wa uovu utafanikiwa siku moja kupindua na kumiliki kwa muda wakati wanaokutazama nao wanapanga njama za kukupindua kupia madhaifu yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…