CCM ni hodari wa siasa

Tanwise

JF-Expert Member
Apr 15, 2015
466
1,032
Miaka imepita tangu CCM iwe madarakani tangu 1992 ndo vyama vingi vimeanza lakini muda wote huo CCM imeibuka kidedea japo kuna chaguzi zilizowahi kuleta upinzani chupuchupu kupigwa chini lakini kwasababu ni hodari waliibuka washindi.

Ni dhahiri hawa jamaa ni wanasisa bora africa kutokea.Yawezekana wanachukua wahitimu au wajuzi wa siasa na kuwa upande wao.Hivyo kila siku kuwa na mbinu mbadala ya kucheza na akili ya wapiga kura.

Upinzani ni kama geresha ya kuongeza democrasia no laasha wamezidiwa kisomo na chama tawala siamini kabisa kwa njia ya rushwa unaweza kununua kura ya mtu makini.

Vizazi na vizazi vitapita na CCM kubaki ni chama bora kiutawala na dunia kushangaa
 
chama kilichokuwa kinategemewa ni chadema, lakn sasa wamejiharibiaga wenyewe kwa kupokea makap
Ni ujinga na upumbavu kusema chadema imejiharibia kupokea makapi, wakati huo unaendelelea kuchagua na kushabikia chama kinachoyazalisha hayo makapi.
 
Mnapokubari vyama vingi hakuna makap. Lasivyo watoto waliozaliwa 1992 kuja huku juu ndo wanapaswa kuwa wapinzani kwa mtazamo wako. Jiongeze jomba
 
watu hawakumwelewa bwm aliposema ccm ikianguka dunia itatikisika, kama nakumbuka vizuri. hii ni kazi iliyotukuka ya gwiji la siasa la afrika, mwana wa afrika, m/kiti wa kwanza wa chama dume ccm, mwl. jk nyerere.
kuna wanasiasa wachache ndani ya ccm ambao wametaka kuivunja misingi aliyoijenga, na hivyo kukidhoofisha chama.
wakati wote chama kimebaini hilo na kurudi njia kuu.
sioni chama cha kuishinda ccm kwa miaka mingi ijayo, hasa hivi vilivyopo vinavyoitaka ikulu kwa maslahi binafsi.
 
Kwa mfumo wa Katiba yetu hata aje Kikwete,Magufuli,Nape na Kinana upinzani bado hautafurukuta.
 
Ni ujinga na upumbavu kusema chadema imejiharibia kupokea makapi, wakati huo unaendelelea kuchagua na kushabikia chama kinachoyazalisha hayo makapi.
makapi ndio , hata kama ccm inazalisha hayo makap kwa weye msafi kwanin uyapokee huku ukijua kabisa hili ni kap, nafikir imefika mda chadema mtambue kuwa mtu aloachwa na ccm keshafulia ck ming angalia akina mrema wako wap sasa kwa mda huu tulonao kuishinda ccm ni kaz ngum vibaya. Tatizo len mnashadadia kushabikia chama ambacho hata ofic ya chama
mikoan pia mabush hakna na huko ndo waliko wapiga kura, pia kumbuka siasa co kama mpira wa miguu #stukaa_best
 
Muasisi wa CCM Mwalimu Nyerere alikuwa genious, alihakikisha kunakuwepo na mpango wa kuwalea wana CCM vijana, ili waje kurithi nafasi za uongozi. Na hao warithi wa kizazi cha Nyerere wanayo hazina kubwa ya uzoefu kwani wamefundishwa siasa mpaka wakaiva. Vyama vingine vimeshindwa kujenga tabia ya kuwaanda vijana ili waje kurithi nafasi za uongozi. Ukiongelea siasa safi CCM wanazifahamu, ukiongelea umafia wa chini kwa chini na wenyewe wanaufahamu vizuri sana.
 
makapi ndio , hata kama ccm inazalisha hayo makap kwa weye msafi kwanin uyapokee huku ukijua kabisa hili ni kap, nafikir imefika mda chadema mtambue kuwa mtu aloachwa na ccm keshafulia ck ming angalia akina mrema wako wap sasa kwa mda huu tulonao kuishinda ccm ni kaz ngum vibaya. Tatizo len mnashadadia kushabikia chama ambacho hata ofic ya chama
mikoan pia mabush hakna na huko ndo waliko wapiga kura, pia kumbuka siasa co kama mpira wa miguu #stukaa_best
Ukiwa ccm lazima uwe mento, ulisha wahi kusikia ccm imemvua uanachama mwanachama wake, tambua kua ccm haiwezi kuuaacha makapi, bali waliochoka huo umakapi ndo wanaondoka ccm tena bila kufukuzwa.
 
Miaka imepita tangu CCM iwe madarakani tangu 1992 ndo vyama vingi vimeanza lakini muda wote huo CCM imeibuka kidedea japo kuna chaguzi zilizowahi kuleta upinzani chupuchupu kupigwa chini lakini kwasababu ni hodari waliibuka washindi.

Ni dhahiri hawa jamaa ni wanasisa bora africa kutokea.Yawezekana wanachukua wahitimu au wajuzi wa siasa na kuwa upande wao.Hivyo kila siku kuwa na mbinu mbadala ya kucheza na akili ya wapiga kura.

Upinzani ni kama geresha ya kuongeza democrasia no laasha wamezidiwa kisomo na chama tawala siamini kabisa kwa njia ya rushwa unaweza kununua kura ya mtu makini.

Vizazi na vizazi vitapita na CCM kubaki ni chama bora kiutawala na dunia kushangaa
Vipi wanaotawaliwa kwa miaka yoote hiyo nao wamekuwa bora kimaisha ,?
 
Utakuwa ume pitiwa ndhani niku rekebishe Heading yako kidogo tu, CCM NI HODARI NA MAHIRI WA WIZI WA KURA,KUBADILI MATOKEO NA KUNYONGA DEMOKRASI KWA GHARAMA YOYOTE.
 
chama kilichokuwa kinategemewa ni chadema, lakn sasa wamejiharibiaga wenyewe kwa kupokea makap
Makapi kivipi? Kama ni makapi mbona wameshinda uchaguzi bara na visiwani ccm mmechakachua, acha hizo akili za Nape mwandosya, mwaka huu ulikuwa mwisho kwa ccm wamepinea kwenye Tundu la sindano.
 
N
Utakuwa ume pitiwa ndhani niku rekebishe Heading yako kidogo tu, CCM NI HODARI NA MAHIRI WA WIZI WA KURA,KUBADILI MATOKEO NA KUNYONGA DEMOKRASI KWA GHARAMA YOYOTE.
na kukandamiza Uhuru wa habari na wapinzani mfano sasa Waziri Nape mwandosya amekuwa dikiteta wa vyombo vya habari yaani ukimkosoa tu lazima akufungie na kukufuta.
 
Ma
Ukiwa ccm lazima uwe mento, ulisha wahi kusikia ccm imemvua uanachama mwanachama wake, tambua kua ccm haiwezi kuuaacha makapi, bali waliochoka huo umakapi ndo wanaondoka ccm tena bila kufukuzwa.
hao wanaowaita makapi waliwapelekesha mpaka wakawa hawapati usingizi, utakumbuka JK alienda na majina mfukoni Dodoma akawadharau kamati kuu ya ccm, mnaowaita makapi leo hii ndiyo wamefanya ccm kuzinduka na kujitambua baada ya kuwapeleka puta kwenye kampeni hadi ukawa wakashinda kwa kishindo lakini ccm wakachakachua matokeo, makapi ni bora kuliko ccm ndiyo maana wametumia pesa nyingi kuwahujumu.
 
Ma
Mnapokubari vyama vingi hakuna makap. Lasivyo watoto waliozaliwa 1992 kuja huku juu ndo wanapaswa kuwa wapinzani kwa mtazamo wako. Jiongeze jomba
makapi ni bora kuliko ccm maana walitumia pesa nyingi kupambana nao kuliko Kipindi chochote tokea Nchi ipate Uhuru.
 
Mkuu ungeeleweka vyema kama ungesema tu kuwa CCM ni mbabe kisiasa hapa nchini.....

Kitu ambacho CCM wanashindwa kutambua ni kusoma alama za nyakati.......hizi ni nyakati ambazo CCM imekuwa ni kichefu chefu masikioni mwa wananchi waliowengi ukiacha wale wachache wanaofaidika na mfumo huu kandamizi......

Upofu wao wa kutokusoma vyema alama za nyakati kumewafanya wasiamini kuwa miongoni mwa matokeo ya uchaguzi ni kushindwa......

CCM WASIPOKUWA MAKINI WATAIPELEKA NCHI KUSIPOTARAJIWA...
 
Back
Top Bottom