Nervousity
Member
- Nov 3, 2017
- 21
- 14
Kwani hoja ya kiserikali hutakiwa kujibiwa na nani? Na hoja ya kichama je?
Kwani mwanachama wa CCM anayo hadhi ya kuwa msemaji wa serikali hata aweze kuijibia serikali? Vipi serikali yaweza kuwa msemaji wa chama kwa upande mwingine?
Vijana wenzangu wa Kitanzania tutaliangamiza taifa letu kwa sababu ya ufinyu na udhaifu wa kifikra wa nini hasa tunapaswa kufanya kama vijana. Umri wetu kama vijana ni mtaji tosha kwa maisha yetu na taifa letu lakini tumekubali ku-behave kama watu wa umri mkubwa ilihali sisi ni vijana. Kwani tumekosa akili kabisa kutuwezesha kujenga msimamo wa maisha yetu ya sasa na ya baadaye? Ni kweli sisi tumekubali kuwa mtaji wa wenye madaraka ya kidola? 'Our future is on our hands!
Kuna mambo ya msingi yanaibuliwa kuikemea au kuihoji au kuitahadharisha serikali lakini ni ajabu iliyoje kijana tena kijana ambaye hajafikisha hata miaka 40 anaibuka na kuanza kutoa matamko, vitisho n.k. Kwani nchi ya Watanzania wote au Watanzania wanachama wa chama cha Mapinduzi tu? Kwa nini hatupo tayari kukosolewa basi hata kutaka viongozi wetu wakosolewe? Kama Rais wetu mpendwa anahubiri unyonge ni sahihi kwa mtazamo wake lakini huo hauwezi kuwa ndio msimamo wa Watanzania wote!
Vijana kuendelea kutetea madhaifu ya kiuongozi yanayoibuliwa dhidi ya utawala wa awamu ya tano ni kudhirisha kwa umma kwamba kuna mengi mabaya ambayo tusingependa yajulikane! Kwani hatma ya maisha ya Watanzania yapo kwa viongozi wa nchi au kwa Watanzania wenyewe?
Vijana tuna-bore! Tunaliangamiza taifa kwa unafiki wetu! TUBADILIKE