Ccm na mbinu chafu

GHIBUU

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2011
Posts
4,432
Reaction score
3,016
KIZAZI CHA NYERERE: serikali ya chama cha mapinduzi imekuwa ikitumia mbinu na hira kudhoofisha upinzani kwa lengo la kujihakikishia kubaki madarakani. mwaka 1995 na mwaka 2000 ilikuwa rahisi kueneza propaganda za kuchafua vyama vya upinzani kupitia Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD). CUF waliwahi kufanyiwa umafia na mwisho wa siku wakabebeshwa na tuhuma kuwa makontena ya visu vya CUF vimekamatwa bandarini sambamba na kudai siasa zao wanafanyia misikitini. hiyo ikawa tosha kabisa chama cha mapinduzi kukichafua CUF na kuendelea kudumu. na katika kipindi hicho vyombo vya habari vilikuwa na mlengo wa chama kimoja na upashanaji taarifa ulikuwa na ubabaishaji mkubwa, uongo kwa lengo la kulinda watu fulani kwa kisingizio cha kulinda amani ya nchi na mshikamano wa kitaifa. Uhuru, Mzalendo, Majira, RTD. matukio ya leo yangejulikana siku tatu zijazo.

KIZAZI CHA INTANETI: serikali ya chama kile kile kikitumia miundombinu chakavu kinapambana na vyama vya siasa kwa mbinu za kidhalimu zenye malengo ya kuweka mazingira ya kuua vyama vya upinzani ili waendelee kunyonya mali na rasilimali za umma wakisahau nyakati hizi habari za kweli tupu zinasambaa kwa kasi na zinaenda kila kona ya nchi yetu. muda wa usambaaji habari ndio kitu kinawamaliza chama cha mapinduzi.
Kama upashanaji habari ungekuwa enzi za RTD basi hivi naongea CUF, CDM na NCCR vingekuwa vimeisha kisiasa maana hata bungeni tusingesikia.

mfano:

1.ishu ya mabomu arusha enzi za RTD nchi nzima habari hii ambayo ingeitwa ugaidi tungeipata saa 2usiku si ajabu lawama zote zingeenda chadema.

2. ishu ya gesi mtwara nchi nzima habari tungepata saa 2usiku na cuf wangeitwa magaidi.

3. kupigwa wabunge wa cdm na nccr (Joshua Nassari na Machalli), kupigwa kwa viongozi wa cuf mtwara hiyo sio habari RTD.

vipi mawazo yako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…