CCM na kosa la kisiasa

CCM na kosa la kisiasa

einsteintz

Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
5
Reaction score
2
Ni dhahiri kabisa, mwaka huu ccm imefanya kosa kubwa kisiasa katika mchakato wa kumchagua mgombea wao wa uchaguzi nafasi ya uraisi. Malamiko mengi ya kwamba mchakato ulijawa na mizengwe mingi pamoja na kuwatarget watu fulani wasiweze kufika mbele kwenye kinyang'anyiro inaonyesha kudhohofika kwa demokrasia ndani ya chama. Katika hali ya kibinadamu hofu sio kitu kibaya hasa unapokumbana na hali ya hatari lakini hofu ya kisiasa kutokana na hatari wanayokaribiana nayo watu wachache si jambo la kuzingatia sana hasa pale ambapo maamuzi fulani yanatakiwa ili kuimarisha mustakabari wa chama. Ni heri demokrasia ingechukuwa mkondo wake kuliko kufanya maamuzi ili kujilinda kisiasa. Watu wanahoji kwamba kama kamati ya maadili ilimkata hata makamu wa raisi Gharib Bilali kana kwamba hana maadili basi utambue kwamba walihodhi mamlaka ya kuchagua wagombea.

#dhana ya umoja ni ushindi ni nadharia tu.

Wengine wanasema uwepo wa makundi umesababisha hayo maamuzi. Lakini kimtazamo tu chama kikubwa chenye historia ndefu na kilichopitia misukosuko mingi kisiasa kingeweza kidhibiti makundi hayo kwa kuwaweka watu chini na kurekebisha tofauti zao. Hii inaonyesha makundi ndani ya chama yamewagawa watu kuanzia ngazi ya shina hadi kiongozi mkuu wa chama kiasi kwamba ni vigumu kupatikana mtu wa kurekebisha hizo tofauti.

Ni rahisi kusema udhaifu ulionyeshwa na bwana mkubwa katika kuongoza nchi umekuwareflected katika kuongoza chama.

#Ngoja tuone ccm itakuja na mikakati ipi.
 
UKAWA Imara! UKAWA Imara!
CCM Makopo! CCM Makopo!

Mimi niliwaambiwa watu jaamani msichukie Mkwere, mkweli ni chaguo la MUNGU, ameletwa na MUNGU ili aje aiue CCM nyie mkawa mnanibishia, sasa naona yale niliyowaambia sasa yanatimia.
Thanks RICARDO KAKA
 
Last edited by a moderator:
Baba akiwa dhaifu kwenye familia ni shidaaaa,wewe uliona wapi mwenyekiti anaingia na viongozi wakuu katika chama mkutanoni, ndio kwanza wajumbe wanaimba wanaimani na mtia nia,hapo tu ni wazi nidhamu kwishenei yaani hajawahi tokea mwenyekiti wa chama dhaifu kama huyo na hapo hayo makundi yenye visasi bado yapo chama chaweza mfia mikononi.
 
Back
Top Bottom