CCM mtawala mbaya

CCM mtawala mbaya

mwanda-mbo

Member
Joined
Jan 16, 2014
Posts
21
Reaction score
3
CCM NI MTAWALA MBAYA
MITHALI 29;2
SIASA ni mfumo wa kimaongozi au njia ya kufanya maamuzi katika jamii, na katika ngazi zote, yaani, Ukoo, Kabila, Jamii, na hata Taifa. Hakuna taifa bila siasa na hakuna siasa bila taifa, hivi vyote vimeumana na vinakwenda sambamba. Moja kati ya sehemu nyeti katika siasa ni majadiliano baina ya watu wenye nguvu au mamlaka na kimsingi katika taifa linalo jiendesha kwa misingi ya demokrasia, basi kila mtu ana sehemu ya nguvu au mamlaka katika kuchangia na hata kufanya maamuzi. Na katika ngazi yeyote ile katika taifa, jamii, kabila, au ukoo, kuna matabaka au mgawanyiko wa vipande viwili yaani wanao ongoza (watawala) na wanaoongozwa (watawaliwa), mifumo ambayo ndio imekuwa ikitwala kwa sehemu kubwa sana duniani.

Kuna mifumo mingi ya kiutawala, kwamfano, utawala wa kifalme –huu ni mfumo wa uongozi unaompa mamlaka ya dola na serikali mtu aitwae MFALME, na katika aina hii ya utawala, madaraka hurithiwa na mtu wa familia ya kifalme. Utawala wa kiimla –huu ni mfumo wa utawala unaotoa madaraka yasio na mipaka kwa kiongozi, na katika aina hii ya utawala, watu baki hawana haki na uhuru katika kufanya maamuzi. Utawala finyu –huu ni mfumo unaowapa watu wachache nguvu za kufanya maamuzi katika dola na serikali, lakini katika utawala huu wachache wanaweza kuwa na nafasi Fulani katika maamuzi lakini tu! Wawe na uwezo wa kiuchumi au nafasi Fulani katika jamii, mathalani ni wanajeshi ila wale wakuu, na kimsingi utwala huu unaitwa utawala wa kikabaila. Utawala wa umma- huu ni utawala unaotokana na umma, yaani jamii inayokuwa inaamua jinsi ya kujiongoza na huu ndio kwa sehemu kubwa ni utawala wa kidemokrasia.

Taifa la Tanzania linalo jinasibu kuwa ni taifa la kidemokrasia, ni kweli kwani makabaila nao hutoa demokrasia kwa wachache wenye nguvu au mamlaka ili kulinda mamlaka kuu, lakini swali kubwa ni kwamba aina gani ya demokrasia ambayo Tanzania inajitapa nayo? Maana ziko aina nyingi za demokrasia, kama demokrasia baguzi, inayo jikita katika kulinda nguvu za kiuchumi; demokrasia duni inyotokana na makundi ya watu na kisha kupitia makundi hayo ya watu huunda serikali; demokrasia shirikishi ambayo wachache hupewa dhamana na wengi katika uwakilishi wa jamii katika kufanya maamuzi na nyinginezo nyingi.

Lakini si dhana yangu kuwapeleka ndani sana kwenye iana za utawala, la hashaa! Nilikuwa nawakumbusha ili tupate kujielekeza vyema katika mada yetu kuu.

Tarehe 20/03/2015, umoja wa mataifa ulikuwa unaadhimisha siku ya furaha duniani, kwa kutolewa ripoti ya furaha katika nchi tofauti ambazo ni wanachama wa umoja wa matifa ikiwemo Tanzania, katika ripoti hiyo ambayo imekuwa kivutio sana kwangu na kunifanya kutafakali maneno mazito sana ya MUNGU katika BIBLIA ya MITHALI 29:2, ‘wenye haki wakiwa na amri, watu hufurai; bali mwovu atawalapo, watu huugua' na kujikuta na swali gumu sana, kwamba inawezekana utawala wa Tanzania chini ya chama cha mapinduzi (CCM), ni utawala mbaya?

Katika ripoti hiyo ijulikanayo kama world happiness report, ambayo imeorodhesha kila taifa limeshikilia nafasi ya ngapi katika bara na hata duniani, na ripoti hiyo ilikuwa ikipima viwango vya furaha vya watu katika mataifa, duniani, na kimsingi furaha hiyo iliyofanyiwa utafiti ilikuwa ikiangazia juu ya utawala bora na kama serikali zinatimiza majukumu yake kwa raia wake ipasavyo? Na mengineyo mengi, kwa maneno mengine tungesema, je! Watu wana furaha na serikali yao kwa namna wanavyo tawala?

Katika ripoti hiyo, iliyo itaja Uganda ndio imechukua nafasi ya kwanza katika ukanda wa afrika mashariki, ikifuatiwa na Rwanda na kisha Kenya, lakini cha ajabu sana eti ripoti hiyo imeitaja Burundi na kisiwa cha amani duniani TANZANIA kwamba watu wake ndio watu wenye huzuni sana katika ukanda wa afrika mashariki na afrika kwa ujumla na hatimae duniani, inawezekanaje taifa linaloogoza kwa kuwa na amani na watu wake wanaishi kwa huzuni? Au hii nayo ni aina ya amani iliyo changanyika na huzuni? chaajabu zaidi ni mataifa ambayo yameshikilia nafasi za juu katika Afrika kama Angola inayoshikilia nafasi ya juu Afrika.

Nilipo anza kutafakali uzito wa maneno hayo na ripoti hiyo nikaogopa sana, kwa sababu moja kati sababu kuu za mapinduzi ya kisiasa katika nchi yeyote ni "common public grief" yaani huzuni ya umma kwa pamoja, kwamba watu wengi wanakuwa hawana furaha tena na utawala ulioko madarakani kwasababu hautendi haki,. Sasa je ni kwamba Tanzania , kisiwa cha amani tumefikia wakati wa kuipindua serilikali ya CCM iliyoko madarakani?

Lakini pamoja na hofu yangu juu ya mwelekeo wa taifa hili kila kukicha kwamba una kwenda mrama, nikaamua kujiuliza; je ripoti hiyo ya umoja wa mataifa ina ukweli ndani yake juu ya Tanzania na sio fitina tu! Kwani kweli Uganda na Kenya ambako kila uchwao watu wanauwawa tena bila maelezo? Eti hadi Rwanda nayo kwao ni safi mbaya zaidi hata Angola nayo imetupita, yaani mataifa haya yana utawala bora kuliko sisi Tanzania?

Lakini kwa msingi wa maneno tulio yaona hapo juu ya kitabu cha BIBLIA katika Mithali 29:2, kwa tafsili yangu ya maneno hayo, ni kwamba, kiashilio kikubwa cha UTAWALA MBAYA katika jamii yeyote ile au taifa lolote lile, ni kuona WATU WAKIUGUA, yaani watu au wananchi husika wanakuwa wanaugua, hawana furaha na utawala ulioko madarakani, na kimsingi, inakuwa kwamba utawala husika unakuwa hautendi haki, umekithili rushwa, ugandamizaji wa haki za binadamu, mauaji ya raia wasio na hatia, na hata tofauti ya walio nacho na wasio nacho kuwa kubwa na mengineyo mengi.

Ni kweli kwamba kila raia anaweza kuwa anaugua na jambo Fulani, lakini kimsingi haya yanayo wafanya watu wa jamii nzima kuumia kwa namna moja au nyingine ni yale ya nayo wagusa watu wengi, mfano athali za rushwa zinamuathili kila raia katika taifa, hivyo basi ili kujua taifa Fulani kuna haki na utawala bora, kwa hakika watu wake watakuwa ni watu wenye furaha na imani kubwa kwa wanao waongoza, na hapa twaweza kuwa na imani kwamba hata amani itadumu.

Tupitie matukio kadhaa yaiyojitokeza katika taifa letu yanayo ashilia mambo si shwari na kuna ukweli kwamba watanzania hawana furaha na wamekata tamaa.

(a) Ajira; taifa hili la Tanzania kupitia serikali ya CCM limeshindwa kabisa kama ambavyo iliahidi katika ilani na sera zake; katika kipindi cha uchaguzi wa 2005 na 2010, kuzalisha ajira kwa watu wake na haswa vijana walio wengi na wasomi, lakini ilikuwa siri sana kana kwamba mambo yako sawa hapo kabla ndipo mwaka 2014 wakati idara ya uhamiaji imetangaza nafasi za kazi 70, na matokeo yake wakajitokeza watu zaidi ya elfu kumi, na bado watu waiopata hizo nafasi ni watoto wa wakubwa (viongozi); yaleyale ya ukabaila. Achilia mbali katika sekta nyingine kubwa ambazo matangazo ya kazi yametolewa na maelfu wakajitokeza na hawakuambulia chochote,; sasa hawa maelfu ya vijana wa taifa hili wasio na ajira na hakika hawana furaha na hakuna matumaini yeyote wanako kwenda, Na nini matokeo ya kundi hili kubwa katika jamii ya Tanzania? Kwa hakika watu hawa hawawezi kuwa na furaha na hata amani, kwani kama kuna njaa utakuwaje na amani?

(b) Raia kuteswa na hata kuuwawa kinyemela, kumeibuka uamaduni mpya katika taifa hili katika miaka ya hivi karibuni, watu kufa tena na vyombo vya dola kama jeshi la jeshi polisi na hata jeshi la wananchi, kwa hili wananchi hawawezi kuwa na furaha, kwani watu wanauliwa na vyombo vya dola kasha wauwaji wanapewa plomosheni na tuzo, huku raia wakishuudia; mfano-tarehe 26-06-2012, Dr STEVEN ULIMBOKA, aliteswa sana na watu wa usalama wa taifa (mwana halisi), huku mkuu wa serikali akisema mbele ya wanchi tena kwa jeuri, LIWALO NA LIWE, yaani akifa potelea mbali; tu kwasababu anatetea kuongezeka kwa dawa na miundo mbinu ya hospitali zetu ili kuwasaidia watanzania, je? Hapa raia watakuwa na furaha? Kwa kile alicho fanyiwa Dr ULIMBOKA, unategemea familia yake wanacheka?, madaktari wenzake nao watakuwa na furaha? Na watanzania ambao tunatarajia huduma kwa hao madaktari, kama wanateswa kwasababu wanatetea hospitali zetu kuwa na dawa za kutosha ili sisi masikini tusio weza kwenda INDIA kutibiwa malaria tupate huduma Muimbili. Pia tarehe 02-09-2012, mwandishi DADI MWANGOSI aliuwawa kinyama na ofisa wa jeshi la polisi, nyororo, kwa amri ya mkuu wake KAMUAHAMBA, kwa makusudi na baadae alihamishwa kinyemela na kupandishwa cheo kama zawadi ya kazi aliyo ifanya ya mauaji, na baadae kustaafu kwa heshima na leo hii anlipwa marupurupu, je? Wananchi wa taifa hili wakuwa na furaha ka jeshi la polisi lina ua hata wandishi wa habari na hakuna haki yeyote, na kudhirisha si baati mbaya kwa ni si mwangosi peekee alie uwawa wapo kama RICHARD MASAU, pia tarehe 05-03-2013 ABSOLOMU KIBANDA nae alifanyiwa unyama kama ule aliofanyiwa Dr ULIMBOKA na watu wenye kufanana na wale wale yaani usalama wa taifa, je? Hapa napo unatarajia watu wafurai?

(c) Kuminywa na kugandamizwa kwa demokrasia, tarehe 05-01-2011, jeshi la polisi liliwapiga raia wa Tanzania waliokwenda kushiki kama ilivyo haki yao ya kikatiba ya kukusanyika; katika mkutano halali wa CHADEMA mkoani ARUSHA, na kuua raia 11, je? Sisi ambao hatukubaliani na sera za CCM hatuna haki ya kuwaunga mkono wale ambao tunaona wanaser zinazo tujali, na je? Kama tuna uawa tu kwa sababu tumeandamana kupinga uonevu, rushwa, tunauwawa na chombo cha dola chenye dhamana ya kutulinda,. Je Tutakuwa na furaha? Na kudhiirisha pia ulikuwa ni mkakati rasmi wa CCM ili kugandamiza demokrasia ni kuuwa kila mwenye mlengo wa fikra za upinzani, jeshi hili la polisi liliendelea kufanya mauaji, kwenye mikutano.

(d) Migomo ya wanafunzi vyuo vikuu, iko migomo mingi sana iliyo tokea hapa Tanzania ikiusisha vyuo vikuu, kiasi kwamba siku hizi tunaita vyuo ni pahala pa mafunzo ya ukakamavu na mapambano kwa vijana ili itakapo fika muda wa Tanzania kuwa kama misri basi hali ya mapambano na jeshi na vyombo vya dola iwe mbaya; ili vijana hawa waweze kuilazimisha serikali kuachia ngazi kwa lazima, februari/2011, wanafunzi wa chuo kikuu cha dare s salaam na januari/2015, wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma nao waliandamana vikali, japokuwa jeshi la polisi lilitumia mabavu sana kiasi kuwaachia vilema wanafunzi waliokuwa wanaandamana kupatiwa mikopo yao, wakambulia mapigo na kuvunjwa viungo, sasa migomo hii inazidi kupandikiza chuki mwa vijana na wengi wa wanafunzi hawa leo hawana matumaini ya kumaliza ua hata kusoma na kufaulu masomo yao, je hawa vijana watakuwa na furaha, kwa sababu migomo hii ndio kiashilia kuwa vijana hawana furaha kabisa.

(e) Maandamano ya machinga, nikisema nitaje idadi siwezi kumaliza, lakini itoshe kusema karibu kila mkoa wa Tanganyika umekumbwa na maandamano ya hawa ambao wengi wao ni vijana, na pengine hili ndio kundi kubwa la vijana katika taifa la Tanganyika wenye gadhabu na hasira kali dhidi ya serikali kwa maonevu na mateso wanayo tendewa na serikali ya CCM, je nani anambie machinga wa nchi hii wana furaha? Hakika hakuna machinga nchi hii anafuraha kwani ndio moja ya kundi la wanchi ya Tanzania wanao ishi kama wakimbizi na wavamizi, huku wakitumika mtaji wa kisiasa kila ifikapo wakati wa uchaguzi na CCM
Kimsingi migomo ya walimu, madaktari, wanafunzi, wafanya biashara, machinga, ikitumika kama njia mpya katika jamii ya watawaliwa kutafuta haki zao tofauti kabisa na utamaduni wa taifa hili, ina dhiirisha wazi kwamba watanzania kwanza hawana imani na viongozi wao na hawana furaha kabisa, ndio maana wameamua kuingia barabarani ili kuandamana kupigania haki zao, ni kama wale wanao amua kuwapiga wezi na kuwachoma moto kuonyesha hawafuraii kabisa tabia hiyo.

Lakini pia imefikia kwamba wananchi wa Tanzania wameamua kuchukua amri mkononi ili kupata haki zao kama wananchi wa arumeru ambao wamempa siku saba mwekezaji kuachilia ardhi yao la sivyo watavamia kwa nguvu, wananchi wa mtwara walioandamana ili wanufaike na gesi, na kimsingi hawa watanzania wa arumeru na mtwara, walichofanya , si kitu kigeni bali ni muendelezo wa utamaduni mpya wa watanzania nchini katika kujitafutia haki zao stahiki.

Sasa kwa msingi huo yote hayo , yanaashilia kwamba watanzania hawana furaha, ndio maana wameamua kutopeleka kilio chao serikalini bali kujipigania wenyewe, kwa hakika hii inatokana na huzuni ndani ya mioyo ya watanzania, na mbaya zaidi serikali ya chama cha mapinduzi imeamua kutumia utamaduni mpya wa mabomu na risasi za moto katika kuwatuliza wananchi wa Tanzania tena bila kuwapatia haki na staiki zao, kiasi kufikia kuua raia wasio na hatia;, kwani mtu aneandamana kudai apewe mkopo amabao ni haki yake, anaambulia kuvunjwa miguu? Sasa afanyaje akajiuze mwili ili apate ada ya chuo? Kwa hakika wanafunzi wa taifa hili pia hawana furaha kabisa.

Nami ANDERSON NDAMBO, sina furaha na utawala wa CCM, kwani hata mwenyekiti wa CCM mteule mfalme wa tanzania, tuliempa dhamana ya kututoa kwenye umaskini; sisi raia tulio kwenye taifa tajiri, kumbe mpaka kufika kipindi cha miaka kumi ya utawala wake hajui hata kwanini sisi raia wake ni masikini? Ili hali akijua vyema Tanzania ni tajiri, ndio maana anaweza kutalii dunia nzima na kwenda kutibiwa tezi marekani, wakati angeweza kutibiwa hospitali ya mwananyamala; na huku raia wake wakikosa dawa na kualala kwenye kitanda kinacho lipiwa lakimbili pale muimbili!

Kwa hayo machache, nihitimishe wazi bila woga na tahashishi, kwamba CCM ni mtawala MBAYA SANA, na umefikia wakati tuukatae utawala mbaya.

MWANDISHI ANDERSON E. NDAMBO, 0718 582371; andambo@yahoo.com
 
Back
Top Bottom