kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 16,252
- 16,171
CCM haihitaji kupaza sauti na kuzuunguka nchi nzima kuelezea mafanikio ya CCM na serikali yake bali kaeni chini mtafakari kilichosababisha mafanikio yenu na kufeli kwenu katika kuwaletea wananchi maendeleo yao. Wananchi wote tunajua kuwa CCM kiliongoza nchi tangu tupate uhuru karibu miaka 50 sasa. Wananchi wote wanajuwa kuwa kama kuna mazuri na mabaya yote yameletwa na CCM na serikali zake. Hivyo, kutembea nchi nzima kuelezea mafanikio ya CCM sio hoja.
Mfano, Wananchi wote tunajua kuwa mafanikio ya utulivu, mshikamano na maendeleo kwenye nyanja mbalimbali kama vile ujenzi wa shule, barabara, hospitali, usafiri, huduma za umeme na maji, ulinzi, vyama vingi, n.k vimeasisiwa na kusimamiwa na CCM na serikali zake. LAKINI pia wananchi tunajuwa kuwa shida za rushwa, madawa ya kulevya, ujenzi holela, kushuka kwa thamani ya shilingi, kupanda kwa bei za vitu, elimu mbovu kwa watoto wetu, biashara za machinga kila kona, mishahara midogo, huduma mbaya za afya, ukosefu wa maji na umeme, wananchi kujichukulia sheria mikononi, ukwepaji kodi, ugonvi wa wakulima na wafugani, waislamu na wakristo n.k pia vimeasisiwa na kusimamiwa na CCM na serikali zake kwakuwa ndio waliokuwa madarakani tangia nchi ipate uhuru.
Kwa maoni yangu hakuna haja ya kuumiza makoo yenu kutuelezea wananchi vitu vilivyofanyika ambavyo ama tunaviona kwa macho yetu, kuvijua ama kuvisikia wenyewe ambavyo vimetokea ndani ya miaka 50 ya uhuru, badala yake tumieni kila dakika na kila senti katika kujadili na kuweka kwenye mizania kati ya mazuri na mabaya yaliyoko au kutendeka wakati wa uwepo wenu madarakani kwa miaka 50 sasa. Badala ya kuzunguuka nchi nzima kuyasema yale tunayoyajua na kuyaona tumieni hizo peza kuongezea mazuri mliyoyafanya kwa miaka 50