Ccm msichukie kukosolewa

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
587
1,000
Anaandika Dr.Chriss Cyrilo (MD)

Sikilizeni vijana wa CCM, tunapomkosoa Magufuli, hatufanyi hivyo kwa sababu ya Uenyekiti wake wa CCM. We have nothing to do with it. Tunamkosoa kwa sababu ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania (Ingawa hatumbui Zanzibar). Tunamkosoa kwa sababu ndie anakusanya kodi zetu, kwa sababu ndiye aliyepata nafasi ya kutekeleza ahadi zake, kwa sababu ndiye anayeishi kwa hisani ya kodi zetu.

Sasa msivimbe mashavu mkadhani tunajali sana mnapokosoa viongozi wa upinzani kwa matusi na maneno ya kutunga, No! Tunawapuuza tu. Viongozi wa upinzani hawakusanyi kodi zenu, hawana nafasi ya kutekeleza ahadi zao, hawana dola, sasa mki-deal nao mnakuwa kama watoto wa nguruwe walionyimwa maziwa na Mama yao, msijue wa kumlaumu.

Na si kweli kwamba mnaipenda CCM saaana, hapana. Ni hulka tu za kujipendekeza kwa watu wenye madaraka ndio zinawaweka huko. Kwa maana hiyo,kama CDM ingeshika dola mngeweza kuhamia CDM kwa sababu hamna fikra kinzani. Na ni kweli kwamba akina sisi tungehamia CCM ili tu kuikosoa, kuielekeza, na kuifunda serikali ya CDM. Wakuda kama nyie hamuwezi kufanya hivyo.

Na lazima mjue, kazi ya kukosoa serikali za kiafrika ni kazi ya kijasiri, mabwege hawawezi kufanya hivyo, ndio maana hatuwezi kukaa meza moja. Tunachoamini sisi, na tunachojua ni kwamba kuna mengi ya kukosoa. Na tutakosoa bila kuogopa kuuawa na kuwekwa kwenye Sandarusi. (No one will get out of this world alive).

Kwa hiyo mfunge mwaka mkijua, Tunakosoa kwa faida yetu na za wakuda kama nyie, mabwege msioweza kujisimamia. Mlishike hilo neno hadi mwisho wa maisha yenu.

Mwisho!
Nothing personal. Me Naandika huku nacheka, ukipata hasira utajizeesha bure.

Dr.Chriss.!
 

Sopa de pollo

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
464
500
CCM siku hizi hawatoi kiki kaka mkubwa, tafuta kitu kingine cha kufanya utatoka tu! One day "yes"
 

kabaka mtesa

Senior Member
Sep 12, 2015
135
225
Kupitia ukosoaji huo baadhi ya wakuda na mabwege wameanza kuishi kwa hisani ya kodi zetu kupitia vyeo vya kuwafuta wakubwa zao jasho.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom