CCM mmetuuzia mbuzi kwenye gunia Igunga

CCM mmetuuzia mbuzi kwenye gunia Igunga

igunga yetu

Member
Joined
Jan 25, 2014
Posts
26
Reaction score
5
Kalamu ya ng'wanangwa kuelekea oktoba 25.

Mwezi juni/julai mwaka huu lililokuwa jimbo la Igunga lilimegwa mara mbili na majimbo ya uchaguzi ya Igunga na Manonga yakazaliwa.

Baadae mwezi julai vyama vya siasa vilianza kutafuta wawakilishi wa Majimbo hayo, kwa upande wa CCM dr. dalaly kafumu (igunga) na bwana seif gulamali (manonga) waliibuka washindi na wameizinishwa jana kupeperusha bendera ya kijani ambapo bwana Samsoni kube (Igunga) na Ndg. Nguzo (manonga) wanatarajia kupitishwa na CHADEMA kupeperusha bendera nyeupe,nyekundu na nyeusi katika maeneo bunge hayo.

Maswali ya kujiuliza kutoka kalamu ya ng'wanangwa kwa mustakari wa majimbo hayo na usalama wa watu wake ni haya yafuatayo;
1. Hawa ni wakina nani hasa?
2. Je, wamekulia na kuyaishi maisha ya wanaigunga wanyonge wa wazawa na majimbo haya?
3. Wanayo nia,mikakati na dhamira ya dhati ya kuwakomboa watu wa igunga?
4. Ni kweli wamepita kwa halali katika kura ya maoni iliyofanyika ndani ya vyama vyao?
5. Wapi kati ya hao wana angalau ya kuwatumikia kwa ufanisi watu wa igunga? Je, ni kafumu na seif ama kube na nguzo?

Ng'wanangwa natua kalamu hii mpaka wiki ijayo tena. Kwa kherini.
 
Back
Top Bottom