CCM mko kwenye wakati mgumu sana wakati huu, jaribuni kusimamia imara.

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,252
8,003
Mmeambiwa kua yeye alienda kuchukua form peke yake, hakusindikizwa na mtu hivyo tumwache asipangiwe cha kufanya.

Mnafikiri angesindikizwa na wanaUKAWA kwenda kuchukua form? Hamjui message inatumwa kwa kina nani? Kama alikua anataka kuwapasha upinzani angeongea mengine na sio sentensi hiyo. Mjifunze sana, siku nyingine mnapochagua tena sikilizeni wengi wanataka nini.

Hili suala la Bahite litawatafuna na kuwagawa vipande vipande, hamtaki kukaa pamoja mkampelekea mapendekezo mwenyekiti wenu mnaogopa kwa sababu mmechimbwa mikwara,chekeleeni tu hamjui.


Kuendesha siasa kwa mbinu za miaka 1980s mtakuja kufahamu tu, mtajua tu hivi sasa ni sayansi na teke linaliwajia.Msipuuze maoni ya wadau, ndio wananchi wenyewe hao.Mpaka sasa mmeshabadili fikra za walio wengi tofauti na mlivyoingia.

Wenzeu hivi sasa wanajipanga namna ya kuwakabilli ninyi na siasa zenu mnazotaka kuanzisha za miaka ya nyuma huku wao wakiwa na mbinu za kisasa.
 
Back
Top Bottom