Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,347
- 26,153
Kama kweli mnaamini kuwa Jaji Warioba amewasaliti,mfukuzeni. Kama kweli mnaamini kuwa Jaji Warioba na Tume yake 'wamepika' Rasimu kwa chuki na hila zao na kuacha maoni ya wananchi kama mnavyodai,mfukuzeni chamani mwenu. Kama kweli mnaamini kuwa mnahitaji muda wa kutosha wa kumkashifu,kumtusi,kumsimanga na kumkebehi Jaji Warioba ndani ya chama chenu,Bungeni na kwingineko,mtimueni chamani kwa kumvua uanachama wake.
Mkifanya hivyo itakuwa poa. Mtakuwa na kila nafasi na muda wa kusema mtakayo juu yake. Wafuatiliaji wa siasa za nchi hii mnatuchosha. Tunawaona ni wa ndimi-mbili kuigiza kumponda Jaji Warioba wakati mnaye chamani.Na mnamheshimu kama Kada mkongwe na mtiifu kwa chama. Kama mmeweza kumfukuza Mansoor wa Kiembesamaki hivi karibuni,mnashindwa nini kwa Jaji Warioba.
Kama hamuwezi,mwacheni Jaji Warioba asimamie anachokiamini. Asimamie Maoni ya Wananchi aliyoyakusanya na Tume yake toka sehemu mbalimbali za nchi hii na kuyaainisha katika Rasimu. Msiendelee na kuonyesha mchezo wa kuigiza.
hawezi kufukuzwa uanachama,lakini hakuna asiyejua kama data na maamuzi yao juu ya rasimu ya katiba yana walakini.mfano mzuri Zanzibar kulikuwa na 2 au mkataba,na neno mkataba na serikali tatu ni maneno yenye maana tofauti kabisa.sasa sijui wao Tatu wametoa wapi!
hawawezi kufanya hivyo kamwe!Kama kweli Komba na wenzie huko Dodoma wanaamini wana hoja basi wamuite Jaji Warioba kwa Q & A.
Mambo yenu ya ufipa yanawashinda mtaweza ya CCM?
Kama kweli Komba na wenzie huko Dodoma wanaamini wana hoja basi wamuite Jaji Warioba kwa Q & A.
WARIOBA NI SHUJAA na kiboko ya ccm , na kamwe jambo la warioba haliwezi kuwa la ccm .
^^
Siri ya Warioba anayo Warioba na Kikwete,, kitendo cha hatua zote za rasimu kuhakikiwa kabla ya uzinduzi rasmi wa Rasimu na ikaruhusiwa kujadiliwa ilihali dola iliyopo madarakani inajua athari zake, isitoshe tuzo ya Muungano akapewa, kinanipa shaka, wanasiasa hawa wanajua CD inayochezwa!
^^
Fukuzeni wazalendo wote basi CCM mbaki na wafisadi