Hali ya kisiasa mkoani Mbeya kwa sasa ni mbaya hali inayompelekea makamo wa Mwenyekiti Philp Mangula kutua tena kesho. Ikumbukwe Mangula alikuwa na ziara mkoani humo ni mwezi mmoja tu umepita.
Chanzo cha habari hizi kimepata ratiba ya Philp Mangula ya siku nane mkoani mbeya inayoanza kesho. Taarifa za ndani zinasema kwamba Mangula anakuja huku kukiwa ni migogoro ya kichama ktk wilaya za Mbozi, Kyela, Ileje, Mbeya vijijini na Mbeya mjini. Hata hivyo Mgogoro mkubwa ni ule wa Mbozi na Ileje ambao unasemekana unapa UKAWA 75% za ushindi kama watasimamisha mgombea.
Kwa mjibu wa taarifa za ndani za chama cha Mapinduzi, wanachama wengi wamedai chanzo cha migogoro yote ni udhaifu wa Mwenyekiti wa mkoa ambaye ameshindwa kuimdu nafasi hiyo na kuishia kuunda makundi ya urais na Ubunge. Zambi ambaye ndiye Mwenyekiti wa mkoa huo wilayani kwake amekabwa koo ilivyo na Kada mmoja aliyefahamika kwa jina moja kuwa ni Mwenisongole ambaye pia ni MNEC wa Mbozi. Taarifa zinasema kwamba hali hiyo inamfanya Mh Zambi kutoelewana na MNEC na Mwenyekiti wa Halmashauri ambao wanamuunga mkono Mwenisongold.
Mgogoro mwingine mkubwa ni ule wa Ileje uliopelekea Mh Zambi na kamati yake ya siasa kuvunja kamati ya siasa ya wilaya ya Ileje akiwepo mwenyekiti. Wachambuzi wa Mambo ya siasa wanasema kuwa kamati ya siasa ilivunjwa ili kufifisha nguvu ya Mh Janet Mbene, Naibu waziri wa Viwanda ambaye inasemekana wananchi wanamtaka achukue jimbo hilo.
Mgogoro huo umekuwa wa aina yake kwani baadhi ya vijiji na mitaa wananchi wamegoma kuchukua fomu za kuwania nafasi za serikali za mitaa. Wananchi waliowengi wanasema kuwa Zambi hawezi kuwachagulia mtu wa kuwasaidia. Wamesema wanasubiria kwa hamu uchaguzi wa serikali za mitaa ili wawapigie kura ukawa kama shinikizo la kupuuzwa. Wameendelea kusema kwamba, hata kama Mbene atanyimwa furusa ya kugombea kamwe hawawezi kuipa CCM Kura na watampa mtu yeyote hata kama ni kivuri.
Tulipomtafta Katibu wa CCM MKOA hakuweza kupokea simu tulipokuwa tunataka kujua udharura wa ziara ya Mangula tena Mbeya, wakati DC wa Ileje alisema hii migogoro imeshanichosha, labda watu wakifa ndipo chama kitasikiliza matakwa ya watu.