CCM maji yako shingoni

gps boy

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2015
Posts
447
Reaction score
65
Kuonyesha kuwa hali si shwari ndani ya CCM baadhi ya Makada wake wameanza kukata tamaa kwani wananchi wanahoji Tania ya Mh. MKAPA kutumia matusi kuomba kura badala ya sera

Hali hiyo imewafanya baadhi ya makanda kumtaka aache kutukana kwani wananchi wanakerwa na matusi take ikizingatiwa alikuwa kiongozi wa taifa hili.
 
mzee ana jazba yule kama kawaida ya ccm wote,jazba ni ishara ya udhaifu
 
Kwa maoni yangu sehemu ilokosewa ni kutumia muda mwingi kumuongelea Lowa na pia kutowaeleza wananchi ahadi za 2010-2015 ni zipi zimetekelezwa; zipi kwenye hatua ya utekelezaji na zipi zitaendelea ktk kipindi cha 2015-2020.

Wenzangu wakaandaa walichoandaa. Ukimtizama jamaa pamoja na mambo mengine ni rahisi sana kueleweka hata kwa mtu wa kijijini. Yaani ni elimu bure mpaka chuo kikuu. Wapi fedha zitatoka; sirikali mwaka jana imesamehe 1.4trn kama msamaha wa kodi.

Mi ninawaomba wanipe 1trn biashara ya elimu bure nimemaliza
 
Kwa hadhi ya mzee Mkapa na hapa namwita mzee sio ati kwa vijisenti vyake bali hakika kiumri ni mzee, unapomsikia akitukana tena wakati anajua wazi kuwa dunia nzima inamwangalia na kumsikia, naona ccm tumekwisha. CCM wameona kuwa hawana tumaini hivyo wakaamua angalao, tushibe matusi tu.

Ndo maana hata yule mjukuu wa mkapa alipopewa nafasi ya kuwatukana babu zake, Magufuli alimpigia makofi. Sera ya matusi sijui inaleta maendeleo gani au inawasaidiaje vijana wetu waliokata tamaa na kuamua kubwia unga na kuwa makontena. This is a shame to this nation.

Naomba msamaha kwa niliyemwudhi
 
Mkapa toka aanze kuwatukana watanzania amepata nini alicho waongezea ccm? au yeye mwenyewe amefaidika nini kwenye maisha yake?

Sema mkapa analaana fulani ivi ambayo inamtafuna kwanza inaonyesha hawa wakina mkapa ndio watu walio cheza dili la kumkausha mzee nyerere na ndio maana uongozi wa mkapa ulipitia misusuko mingi kuungua ikulu mkapa kuvunjika mguu nk.

Na hata mpaka leo ukimuangalia vizuri ni kama mtu ambaye amechanganikiwa na hana akili vizuri. Na ameshindwa hata kuiheshimu demokrasia.
 

Hapo umegonga penyewe mkuu. Chief strategist wa kampeni za ccm ni hopeless sijapata kuona. Haya unayoyasema yalipaswa kuwa kwenye mabango yao nchi nzima.

Cha ajabu mabango yao yamejaa picha za mtu (ambaye hata ndevu hakunyoa kabla ya kupigwa picha) as is ccm haijawahi kuwa madarakani na hakuna ilichofanya kwa miaka 54.

Mnatuwekea mabango mpaka chooni na hayana content yeyote halafu mnatuambia hamna pesa za madawati,maabara na madawa? Ni mwendawazimu pekee ndio anaweza kufanya haya. Na kwa hili nimewachukia zaidi ccm.
 
Viongozi wa ngazi za juu wameshiriki kwa kiasi kikubwa sana kuiua CCM!
 
Wewe hueleweki mara unajipambanua kama CCM mara unageuka na kuwasema kama outsider.
 
Wewe hueleweki mara unajipambanua kama CCM mara unageuka na kuwasema kama outsider.

Tata;
Magufuli unamwelewa?? Miye simweliwi kabisaa namwona ka mgombea binafsi au mtu ambaye hakuwa kwenye system
 

usisahau na yale mapesa wanayomwaga kwa wanaoitwa wanamuziki.
 

imenishangaza sana pale zanzibar airport, lile screen kubwa ambalo lilitakiwa lionyeshe arrival and departure time za ndege naona linaonyesha kampeni za ccm, ukifika tu unakutana na kijani kwa njano ati mtaisoma namba, sasa sijui hao watalii wanaoingia ndio wataisoma namba, nimeshindwa hasa kuelewa
 
watalii hawaji sasa hivi mpaka uchaguzi ukae sawa
 
"Mwanaume unataka mabadiliko?. Kabebe mimba"-Mkapa

Maneno haya yangekuwa kweli TAMWA wamekuwa wamekwisha toa TAMKO.

This is very ant gender statemener. wanaobeba mimba ni watukuka, wana nafasi maalumu katika Taifa and they are not the condemned ones! Wapeni akina mama heshima yao.

Kwa Wanaume Wazungu mwanamke akiingia ndani husimama kutoa heshima. Asiyejua hili aende Matenity Ward akushuhudie ujasiri wa wanawake, Hats off to women.
 
Tumeichoka kabisa CCM..kama ungekuta ni lidude lenye kupumua..wacha lifilie mbali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…