Gamba la Nyoka
JF-Expert Member
- May 1, 2007
- 7,022
- 9,292
Wakati wa ukatibu mkuu wa Mzee Makamba, Chama cha Mapinduzi kiliporomoka umaarufu kwa kasi ya kutisha hadi kufikia hatua wanachama wao wenye kupenda kuvaa nguo za rangi ya chama kuzomewa, kudhihakiwa na kubezwa, hali hii ikafanya CCM wabadiri timu kwa kumuondoa mzee Makamba na kumleta Willison Mkama, ambaye naye hakusaidia sana kubadirisha hali. Hii ilipelekea CCM kufanya mabadiriko na kumleta mzee Kinana, Kupitia kwa Kinana na Nape Nnauye walipiga kazi nzito ya kuzunguuka takriban kila wilaya ya nchi hii kuinua uhai wa chama, Angalau sasa chama kikapata heshima iliyokuwa imepotea.
Msingi wa juhudi hizi uliisaidia sana CCM katika uchaguzi wa mwaka 2015.
Hata hivyo CCM ilipata boost ya umaarufu kupitia kwa Raisi Magufuli ambaye rekodi zake za uwaziri hususan ujenzi wa mabarabara ulikiinua chama, na wabunge wengi wa CCM walipatikana kupitia jina la Rais Magufuli
Hata hivyo kwa yanayoendelea nchini kwa sasa ambapo tunaona Kiusalama kuna hali ya Sintofahamu, Watu wanatekwa na wengine kupotea katika hali ya utatanishi.
Tukiangalia Operesheni mbalimbali kama zile za uhakiki wa vyeti vya elimu ambapo aatu wamefukuzwa kazini, wengine wamehukumiwa vifungo jela, Lakini kuna mtu anatuhumiwa kufoji identity na kutumia vyeti cya mtu mwingine, huyu haguswi na inaonekana anakingiwa kifua hii imezua hali ya chuki kali kwa watu dhidi ya serikali yao, nimefuatilia mitandao, nimekaa vijiweni nimesikia watu wanayoongea kwa kweli watu wamechukizwa.
Lakini tukiangalia hali ya kiuchumi ambapo ajira zinazotengenezwa kila mwama lulinganisha na ajira zinapaswa zizalishwe kila mwaka ni ndogo sana, Serilali imesema imetengeneza ajira 400000 lakini kila mwaka zinahitajika ajira Milioni 1.6, maana yake watu Milioni 1.2 hawapati ajira kila mwaka, maana yake baada ya miaka mitano Watu milioni Sita waliopaswa kuajiriwa ktk awamu hii ya utawala watakuwa hawana ajira, hili ni bomu jingine linalosubiri kupasuka
Lakini pia hali ya chakula nchini na uwezo wa wananchi kudhindwa kukinunua, hii yote ni disaster.
Cha kuiumiza CCM, Nguvu na Energy aliyokuwa nayo mzee Kinana miaka mitatu iliyopita siyo sawa na sasa, ni dhahiri Kinana alipoomba kustaafu alishajiridhisha kuwa kwake inatosha!
Sasa ni dhahiri kwa hali ya mambo inavyokwenda, Chama cha Mapinduzi kitajikuta kinaporomoka zaidi kiumaarufu kuliko hata nyakati za mzee Makamba!, na hii inaweza kupelekea CCM ikapoteza uchaguzi wa mwaka 2020.