CCM kumwajibisha mbunge wake aliyemgawia mpinzani muda wake kuchangia bungeni

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885
Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde amesema kitendo alichofanya Mbunge mwenzake wa Jimbo la Mara CCM, Boniface Getere cha kugawana muda na mbunge wa Serengeti (Chadema), Marwa Ryoba ni utovu mkubwa wa nidhamu.

Lusinde ni mmoja wa wabunge wa CCM waliomlalamikia Getere kumpa dakika tano Ryoba ili aweze kuchangia taarifa za kamati za Bunge Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii na ya Kilimo, Mifugo na Maji baada ya mwenyekiti wa Bunge, Mussa Hassan Zungu kumruhusu azungumze kwa dakika kumi.

“Duniani kote kazi ya upinzani ni kuipinga Serikali iliyopo madarakani na kazi ya wabunge wa chama tawala ni kuishauri Serikali na kuipongeza pale inapofanya vizuri, hizi ni kambi mbili tofauti,huwezi kuwapa muda wapinzani” amesema Lusinde.

Naye mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea amesema haoni ubaya kwa mbunge wa CCM kumpa muda mbunge wa upinzani bali anachokiona CCM wanahamishia kampeni bungeni.

Hata hivyo, alipoulizwa Getere iwapo haoni kama amefanya makosa kumgawia mbunge wa upinzani, amesema hajaona madhara yoyote kwa kitendo chake hicho.

IMG_20170211_044201.jpg
 
Wamekuwa Marafiki huko Bungeni
kisa Makonda kutaja majina!!!
Hapa utagundua Kwenye Mambo yamuhimu kwa watanzania Hawana umoja
ila kwenye Kitonge chao kinacho wateketeza Watanzania Wanaungana!!!

Sasahivi Chenge kawa Malaika Bungeni!!
Watanzania Tuna picha za wabunge Siyo wabunge
 
Ndo maana nilishangaa pale walipoungana kumuita Makonda. Toka lini hawa watu wakapatana lazima kuna kitu.
 
Kwa hoja hizo alizozitoa Rusinde,sishangai kwa nini hadi sasa jimbo lake linaamini kuna watu wananyonya damu za wenzao.Huko ndiko watafiti walipovamiwa na kuteketezwa kwa moto wakihisiwa kuwa ni wanyonya damu.

Si kwamba ccm imeufanya mkoa huo kuwa makao makuu ya nchi kwa bahati mbaya,hapana ni kwa sababu una aina ya watu wanaishi na kuamini mambo ya karne ya 17,kama mkuu wa nchi aliwahoji Wanakagera kuwa kwa nini kila baya lianzie kwao,kwamba ukimwi ulianzia kwao,tetemeko kwao,wana mto unaitwa mto ngono,na kijiji kiitwacho katerero,kwa nini asitumie nafasi yake tena kuwahoji wana Dodoma maswali ya aina hiyo?

Ni wakati wa kuwahoji wanadodoma kwa nini kila jambo la kipuuzi liwe kwao?Hospitali ya milembe ipo Dodoma,wala viwavi jeshi wapo Dodoma,wala ugali wa njano wenye sumu wapo Dodoma wanaouwa wenzao kwa kuwadhani ni wanyonyadamu wapo Dodoma,waropokaji bungeni wanatoka Dodoma,hata ombaomba pia wengi wanatoka Dodoma.Kuna nini Dodoma?

Kwa sifa hizi sishangai kwa nini Dodoma imefanywa kuwa makao ya serikali,bali nashangaa kwa nini wanadodoma hawajawahi kuulizwa maswali hayo na mkuu,badala yake alienda kuwauliza Wanakagera.Ni maswali yenye ukakasi lakini yaliasisiwa na mkuu wetu kule Kagera,yaulizwe tu kwa wanadodoma.CCM hoyeee!!!!
 
Hivi kikatiba wabunge wa upinzani na chama tawala wametofautiana majukumu?

Sijamuelewa LUSINDE hapa.

“Duniani kote kazi ya upinzani ni kuipinga Serikali iliyopo madarakani na kazi ya wabunge wa chama tawala ni kuishauri Serikali na kuipongeza pale inapofanya vizuri, hizi ni kambi mbili tofauti,huwezi kuwapa muda wapinzani” amesema Lusinde.
 
Back
Top Bottom