CCM kukosa dira ya maendeleo Tanzania

CCM kukosa dira ya maendeleo Tanzania

niester

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2012
Posts
254
Reaction score
111
Nimekuwa msomaji mzuri wa Jamii forum na kuchangia mada mbalimbali , sasa na mimi leo nimeamua kuleta uzi huu ili kuona jinsi gani viongozi na sera ya CCM inavyodanganya watanzania.
Mwaka wa uchaguzi kuna ahadi ambazo hata mtoto wa darasa darasa la kwanza Ukimwambia hii ahadi anaweza kusema hii ni ahadi ya "kufikirika"
Hakika kila jambo lina mwisho wake na ukiona mwisho wake hapo ndo unajua kbs kuna mambo mabaya yanatokeaa.
Walimu wa tanzania hawahitaji laptops kwa ajili ya kufundishia. Walimu wanalalamikia mazingira mabovu ya kufanyia kazi ikiwemo ,malimbikizo ya mishahara, hawapandishwi madaraja richa ya kuongeza elimu juu, upungufu wa nyenzo za kufundishia, vyoo vya shule vibovu,nyumba mbovu n.k mbaya zaidi walimu wanadharauliwa na viongoz wa serikali kwa mfano ile kauli ya Mwantumu Mahiza alisema"kama mnaona kazi ya ualimu hailipi acheni kazi mjiunge na siasa " na ile ya mkuu wa nchi alisema " hata mkiandamana miaka 8 mishahara haiwezi kuongezeka ".- Leo hii ilani ya CCM na mgombea urais inakuja na propaganda za ajabu "Eti nikishinda nitagawa laptops kwa kila mwalimu na nitatoa 50 milioni kwa ajili ya maendeleo kwa wananchi".- Hivi kweli hawa CCM wanajua kutengeneza laptops za solar power na kuwagawiya walimu inchi nzima kuanzia chekechea,shule ya msingi,sekondari Itagharamu shi ngapi?.Hivi hawa ccm na sera zao wamesahau kuhusu yale mabilioni ya kikwete yalivyotesa wananchi kila mkoa?je wanaweza kutuambia yale mabilioni ya kikwete kuna mradi wowote wanaoweza kujivunia kuwa umesimama na kuendelea? Leo hii wanakuja na ahadi ingine ya kugawa pesa kwa kila kijiji kwa ajili ya maendeleo. Uliona wapi kwa nchi zilizoendelea serikali inagawa pesa kwa wananchi ili waendelee?ama kweli CCM imepoteza dira na inaelekea kufa.
Magufuli ni kiongozi mzuri lkn ukiangalia kiundani kbs ni mtu ambaye hakujiandaa kuwa raisi na ndyo maana kwa sasa wanahaha na ahadi hewa. Magufuli yupo kwenye mfuko ambao ni corrupt hata akiingia madarakani itabidi aulinde na kutekereza sera ya CCM.
Pamoja na kwamba Lowassa anazongwa na kashfa ya Richmond lkn wananchi sasa wameshajua nini kinaendelea ndyo maana wanamuunga mkono kwa gharama yoyote.
Japokuwa CCM wanasema watashinda kwa namna yoyote ile hata kwa goli la mkono lakn tunasema.
Viva Ukawa viva lowasa,viva wananchi
Huwezi kuyazuia mafuriko kwa mkono na ushindi ni asubuhi na mapema October 25-
Tukutane October, 25 saa nne asubuhi
 
Hahaha! Tukutane October 25 saa nne asubuhi, imetulia hiyo.
 
Tutawanyoosha hadi wakome wewe subiri tuu@kinyasi
 
Nampenda magufuli sema hii ya laptop kama kakurupuka hivi kazi anayo

Si bado serikali ya chama cha mapinduzi ipo madarakani kwani laptop zimeisha madukani na je viwanda china vimefungwa.si wazichukue hata kwa mkopo wagawe wanasubiri nini?mbona wanatuchanganya hawa?
 
Laptop ntawapa jamani,Sitawaangusha;by Magufuli
Hahahahahahaaaa jamaa hafai huyu
 
Si bado serikali ya chama cha mapinduzi ipo madarakani kwani laptop zimeisha madukani na je viwanda china vimefungwa.si wazichukue hata kwa mkopo wagawe wanasubiri nini?mbona wanatuchanganya hawa?


Nimeipenda hii
 
Back
Top Bottom