TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,742
Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kilimanjaro kimedai kushangazwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe jinsi anavyomkosoa Rais Dr. John Pombe Magufuli.
Kwa mujibu wa chama hicho, kitendo cha Mbowe kuwa mstari wa mbele ili kuwatetea watumishi wazembe, wabadhilifu na mafisadi waliofukuzwa au kusimamishwa kazi kutopewa nafasi ya kujitetea , inaonesha kiongozi huyu ni miongoni mwa MAJIPU yanayohitaji kutumbuliwa na rais Dr. John Magufuli.
''Mtumishi wa Umma anayetuhumiwa kwa tuhuma yoyote taratibu zinaruhusu kusimamishwa kazi, kupisha uchunguzi, akikutwa hana kosa anarudi kazini'' Alisema Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Deogratius Rutta.
Chanzo: Majira