CCM itaruhusu mgombea urais kushindana na Magufuli mwaka 2020?

mkafrend

JF-Expert Member
May 12, 2014
3,047
1,503
Wanajf, salaam!
Chama cha MAPINDUZI ni chama kikongwe na imara si tu nchini bali barani Africa. Nachojiuliza ni je iwapo wakijitokeza makada wa CCM kutaka kugombea nafasi ya urais mwaka 2020;
1. Je, CCM iko tayari kuwaruhusu?
2. Je, hii unaweza kutafsiriwa na viongozi wa juu wa chama na serikali kama kumkosea heshima Mhe. Rais hasa pale atakapopenda kuendelea?
3. Je, msimamo wa mrithi wa NNAUYE aliyekuwa mpigania haki, usawa na maazimio ya Arusha utakuwa upi?

Taifa ni muhimu
Nchi ni muhimu
Vyama vya siasa ni muhimu
Wanachama ni muhimu pia!!!
 
Ni Shibuda sio Jidulamabambasi huyo alikuwa CUF
John Shibuda alifanyaje?

Yeye aligombea na JK kura za maoni 2005 na hakuwa pekee yake kulikuwa na Salim Salim,Idd Simba,Frederick Sumaye(alipokatwa ndiyo akaenda kusoma aliyemchezea rafu alikuwa Lowassa siku hizo,yy hakuingiza jina),Pro:Mark Mwandosya n.k(kwa kutaja wachache)

Pale CCM aligombana na misimamo Bungeni lilipokaribia kumalizika (2010),akarukia CHADEMA nako akawaburuza kwa kuwaambia Ubunge nimeupata kwa jina langu,pia misimamo ya kugoma hakuikubali.

2015 akahamia ADA TADEA akagombea Ubunge akaukosa.Ila ni Kiongozi wa Juu.
Chama chake kimepata Mwakilishi wa kuteuliwa ZNZ na kupewa Uwaziri,kwani kilishiriki Uchaguzi.

Kipindi chote alilishika Jimbo la Maswa..

Km kuna makosa tusahihishane ndiyo maana ya kuwa pamoja.
 
Back
Top Bottom