CCM inazidi kugawanyika

CCM inazidi kugawanyika

Nikukumbushe

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2013
Posts
2,602
Reaction score
408
Ama kweli kila lililo na mwanzo halikosi kuwa na mwisho. Kitendo cha aibu alichofanyiwa Jaji Joseph Warioba ni kundi lingine linaloibuka ndani ya CCM,ni kundi la wazalendo wa kweli,ni kundi la watu wenye busara,ni kundi la watu waliofanya kazi karibu sana na mwalimu Nyerere.

Nakumbuka siku ya mdahalo,Warioba alisema,kuna watu wanatumia vibaya jina la mwalimu katika kufanikisha maslahi yao. Ni mwalimu huyu huyu tuliyefanya naye kazi au ni mwalimu mwingine?

Alihoji Warioba.
Warioba alisema,mwalimu amekufa akiliamini na kulitetea azimio la Arusha. Je,mwalimu angekuwepo angeruhusu watu kuwa na akaunti nje ya nchi,mwalimu angekuwepo angepinga uwepo wa maadili ya viongozi kwenye katiba,alihoji Warioba. Au mnamzungumzia mwalimu mwingine sio huyu ninaye mfahamu na kufanya naye kazi.

Kauli ya Sitta.
Sitta yeye anasema,Warioba alijitakia. Kwa tafsiri yake ni kwamba kilichomtokea Warioba kilistahili. Sitta anasahau kuwa yanayotokea hapa kiini kikubwa ni yeye. Kauli ya Sitta ni ya kulaaniwa na mtu yeyote aliye na utu na anajali utu wa wengine.

Kauli ya W. Malechela.
Yeye anasema,iweje mtu yuko CCM aendelee kupinga serikali? Iweje aendelee kupinga wakati anapata mafao yake kwa mgongo wa CCM? Alihoji.Ninachokijua mafao ayapatayo Warioba ni haki yake kikatiba na sio suala la U-CCM.Nauliza swali,je iwapo Warioba atarudisha kadi ya CCM mafao yake yatasitishwa au ataendelea kupewa?

Bali na kundi la Warioba,kuna kundi la mbabe Sitta,Lowassa,Membe nk.
CCM lazima ife,na hii ni dalili za kuanguka kwa CCM. Kipimo ni katika chaguzi zijazo. CCM haiwezi kuwadharau,kuwapiga,kuwatukana,kuwakejeli wazee wenye heshima na busara ikabaki salama,hakuna.
 
Mkuu umemaliza kila kitu lakini nijuavyo mimi ccm ni sikio la kufa,watakuja hapa wale viroboto wa lumumba na kutoa kila aina ya uharo lakini ukweli ndio huo! Ni suala la muda tu
 
Niliahidi.jpg

profilepic 2015.JPG

mizambwa
inaniuma sana!!!
 
Sitta ameisha laaniwa na amelaanika! maana unaweza kulaaniwa usilaanike, laana zingine ni hila tu! lakini ajue kujifunza, yamemkuta menigi amebaki ujingani tuuu? ajue kwamba What goes around comes around" Atajutia maana alipewa nafasi ya kuwa mkamilifu akaipotosha na sasa amewatengenezea watanzania kaburi la nchi, asubiri aone laana hii itakavyomfuata. Yeye awaombe radhi maaskofu lakini mungu wetu wa haki yu juu ya hao maaskofu.
 
Buku saba Fc mpo wapi nyumba inaungua huku.
 
Ama kweli kila lililo na mwanzo halikosi kuwa na mwisho. Kitendo cha aibu alichofanyiwa Jaji Joseph Warioba ni kundi lingine linaloibuka ndani ya CCM,ni kundi la wazalendo wa kweli,ni kundi la watu wenye busara,ni kundi la watu waliofanya kazi karibu sana na mwalimu Nyerere.

Nakumbuka siku ya mdahalo,Warioba alisema,kuna watu wanatumia vibaya jina la mwalimu katika kufanikisha maslahi yao. Ni mwalimu huyu huyu tuliyefanya naye kazi au ni mwalimu mwingine?

Alihoji Warioba.
Warioba alisema,mwalimu amekufa akiliamini na kulitetea azimio la Arusha. Je,mwalimu angekuwepo angeruhusu watu kuwa na akaunti nje ya nchi,mwalimu angekuwepo angepinga uwepo wa maadili ya viongozi kwenye katiba,alihoji Warioba. Au mnamzungumzia mwalimu mwingine sio huyu ninaye mfahamu na kufanya naye kazi.

Kauli ya Sitta.
Sitta yeye anasema,Warioba alijitakia. Kwa tafsiri yake ni kwamba kilichomtokea Warioba kilistahili. Sitta anasahau kuwa yanayotokea hapa kiini kikubwa ni yeye. Kauli ya Sitta ni ya kulaaniwa na mtu yeyote aliye na utu na anajali utu wa wengine.

Kauli ya W. Malechela.
Yeye anasema,iweje mtu yuko CCM aendelee kupinga serikali? Iweje aendelee kupinga wakati anapata mafao yake kwa mgongo wa CCM? Alihoji.Ninachokijua mafao ayapatayo Warioba ni haki yake kikatiba na sio suala la U-CCM.Nauliza swali,je iwapo Warioba atarudisha kadi ya CCM mafao yake yatasitishwa au ataendelea kupewa?

Bali na kundi la Warioba,kuna kundi la mbabe Sitta,Lowassa,Membe nk.
CCM lazima ife,na hii ni dalili za kuanguka kwa CCM. Kipimo ni katika chaguzi zijazo. CCM haiwezi kuwadharau,kuwapiga,kuwatukana,kuwakejeli wazee wenye heshima na busara ikabaki salama,hakuna.

Sitaa, Membe, Lowassa, Chenge ni majanga makubwa kwa mustakabali wa taifa letu. Hawa watu wanataka kuwa marais wa nchi hii mbona tutalia sana. Hakika tukatae kuwapitisha watu hawa.
 
R.I.P wasakatonge walikupenda lakini mungu kakupenda zaidi!
 
CCM hata siwaamini hata kidogo,nikisema warioba apewe ulinzi zaidi nafsi yangu inanisuta maana hao hao walinzi wanaweza kumgeuka.
Hatutaki,na hatutegemei Jaji Joseph Warioba yamkute kama yaliyomkuta Dr.Sekondo Mvungi(R.I.P)
 
Back
Top Bottom