CCM Inawezaje Kuacha Kuwa Ombaomba?

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu zangu,

Juzi nilifuatilia Mkutano Mkuu wa dharura wa CCM kule Dodoma. Usiku huu, na tayari ni Jumatano, nimeyapitia magazeti ya Jana.

Kama ilivyotarajiwa, mengi yameandika juu ya yaliyotokana na mkutano ule lakini zaidi yenye kuzungumzia watu.

Swali kubwa jana ni je, kuondoka kwa Sophia Simba na wenzake CCM kutaiathiri CCM? Na swali lingine, Je, wakihamia upinzani, inawezekana kwa upinzani kuimarika zaidi?

Kwa mtazamo wangu, na kwa nilivyojitahidi kuzielewa siasa za nchi hii, Sophia Simba na wenzake yawezekana kabisa ni ukurasa uliofungwa kwenye simulizi za ushiriki wao wa siasa za nchi hii kupitia CCM na hawatakwenda kwengine. Yumkini ukafunguliwa ukurasa mpya katika siku zijazo, wakiwa ndani ya CCM hiyo hiyo. Kwamba aina ya watu waliofukuzwa, kuhamia upinzani yanaweza kuwa maamuzi magumu watakayokuwa wameyafanya na kuwa tayari na gharama zake.

Kwangu, swali muhimu linabaki; Je, CCM inaweza kuacha kuwa ombaomba?

Moja ya mazingira yaliyokifikisha Chama Cha Mapinduzi hapa kilipo leo, na changamoto zote inazozikabili, ni ukata. Hali ya kuwa chama kikubwa, lakini, kisicho na uwezo wa kujitegemea kiuchumi kiasi cha kutegemea fedha za wafadhili hususan wafanyabiashara.

Ikumbukwe, CCM ilipata hata kuwa na Shirika lake la Uchumi- SUKITA. Watu wa aina ya Bwana Kapinga ndio waliopewa dhamana ya kuongoza SUKITA. Huku wakilindwa, walihujumu SUKITA.

Juzi Mwenyekiti wa CCM, John Magufuli amesikika mkutanoni akisema; kuwa pamoja na utajiri wa chama hicho, bado kimeendelea kuwa ombaomba na kupokea fedha kutoka kwa watu wasiostahili.

Mwenyekiti wa CCM Magufuli yuko sahihi. Na ukweli mwingine mchungu ni kuwa watu hao hao wasiostahili ndio wamekuwa wakitumia fedha zao, kuwaweka viongozi wasiostahili kuanzia ngazi za Udiwani hata Ubunge. Na wakati mwingine, wametumia fedha zao kujiweka wenyewe kwenye nafasi za uongozi kwa kuwahonga wapiga kura.

Mabadiliko makubwa na ya kweli kwa CCM, ni pale Mwenyekiti wa Chama hicho, John Magufuli, kama atafanikiwa japo kwa asilimia 80 tu, kuhakikisha wagombea wa nafasi mbali mbali za uongozi kutoka chama hicho, kuwa wapatikane bila matumizi ya fedha za kuhonga wapiga kura au watendaji wengine kwenye hatua za kupatikana wagombea. Hayo yatakuwa, sio tu mabadiliko makubwa, bali mapinduzi makubwa.

Kwenye Mkutano Mkuu ule wa Dodoma tulimsikia pia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitolea mifano ya vyama vya siasa vya China na Afrika Kusini; CCP na ANC.

Kuna chama ambacho nilishangaa Kinana hakukitolea mfano, lakini, ndicho chama ambacho CCM inapaswa kujilinganisha nacho pia, na kuona aibu. Ni Frelimo.

Frelimo sio tu chama rafiki na CCM, ni chama ndugu. Kwanini Frelimo imeweza kuwa chama kinachojitegemea kwa kupitia rasilimali zake na CCM imeshindwa?

Hivi ni wangapi wanaojua kuwa Frelimo, iliyopewa makazi yake na TANU hapa Tanzania inamiliki zaidi ya nyumba 140 katika jiji la Dar Es Salaam. Sina takwimu nyingine ya rasilimali za Frelimo hapa nchini, lakini, nina imani zipo.

CCM inapaswa kujifunza nini?

CCM ingeziwahi fursa za kuwekeza nje ya mipaka on auspicious ya kuvisadia vyama vya ukombozi. CCM leo ilipaswa kuwa na vitega uchumi Namibia, Msumbiji, Afrika Kusini na hata Angola. Kizazi kile cha viongozi wapigania uhuru bila shaka wasingesita kuweka mazingira ya CCM kuwa na vitega uchumi hivyo kwenye nchi zao. Ikiwa kama shukrani zao kwa yote waliyofanyiwa.

CCM ilikosa nini?

Strategists, strategists, strategists- Wapanga mikakati. Nahofia, kuwa tatizo hilo bado wanalo CCM, hata leo.

Ni nafasi nzuri ya Mwenyekiti wao mpya, John Magufuli, kukielekeza Chama Cha Mapinduzi kwenye misingi mipya ya kujitegemea kiuchumi ili kibaki kuwa ideology party- Chama Cha Kiitikadi na chenye kwenda na mfumo wa soko kama ilivyo kwa CCP, ANC na Frelimo. Hiyo ndio itakuwa CCM mpya. Kwa mtazamo wangu.

Maggid Mjengwa.
 
Mpaka sasa 99% ya assets za CCM ni Mali ya Serikali, zilipatikana enzi ya Chama na Serikali. Hivyo kuna haja ya kupeleka kesi Mahakamani kudai raslimali hizi zirudishwe serikalini period.Mengine hayatuhusu hata kikifa leo ni sawa tu hakina faida yoyote.
 
Majjid, CCM itajitegemea pale itakapoacha kutegemea serikali. Kuacha kutegemea matajiri wakati unategemea dola kufanya shughuli zako, wote ni utegemezi. Mabadiliko ya wiki iliyopita yamekiondoa rasmi chama mikononi mwa makada na matajiri na kukikabidhi mikononi mwa polisi na usalama. CCM ya sasa yaweza kuacha omba omba kwa matajiri, lkn haiwezi kuacha omba omba hazina na kwa vyombo vya usalama. Nambie, ilikuwa inawahusu nini polisi kuwakamata kina Bashe huko Dodoma kama si polisi kujiingiza katika siasa za ndani ya chama?
 
Kuwaza Utajili uliopolwa kwa Wananchi na ni mali za nchi sio sawa vyama havitakiwi kuwa bepari luzuku tu yatosha mali zisizo hamishika za nini? zikiwa za serikali ndio sawa... ili kusiwe na ugomvi mbeleni... Tumeona ya Timu za Mpira kama Nyota Nyekundu,Pan African na Saigon mali kama hazina wenyewe zimelambwa tu na wajanja hizi mali huwa hazina umiliki zikiwa za serikali ndio zinakuwa mikono salama. Tumeona viwanja vingi vya wazi ni utaperi tu vikageuka vya ccm bila maelezo na hata Hati hawana.
 
Majjid, CCM itajitegemea pale itakapoacha kutegemea serikali. Kuacha kutegemea matajiri wakati unategemea dola kufanya shughuli zako, wote ni utegemezi. Mabadiliko ya wiki iliyopita yamekiondoa rasmi chama mikononi mwa makada na matajiri na kukikabidhi mikononi mwa polisi na usalama. CCM ya sasa yaweza kuacha omba omba kwa matajiri, lkn haiwezi kuacha omba omba hazina na kwa vyombo vya usalama. Nambie, ilikuwa inawahusu nini polisi kuwakamata kina Bashe huko Dodoma kama si polisi kujiingiza katika siasa za ndani ya chama?
Bashe alikataa hakukamatwa na police
 
Back
Top Bottom