CCM- Inahitaji Naibu Katibu mkuu Mwingine

CCM- Inahitaji Naibu Katibu mkuu Mwingine

anney

Senior Member
Joined
Jul 9, 2010
Posts
155
Reaction score
45
Salamu zangu za mwisho wa mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka 2013 kwa CCM ni kuhusu nafasi ya naibu katibu mkuu wake Mwigulu Chemba. CCM inahitaji kumtafuta mtu makini mwenye uwezo wa kujenga chama na kufahamu taifa linataka nini kuelekea mwaka 2015. Rafiki yangu Mwigulu ni Janga Ndani ya CCM na mstakabli wa chama chake na amani ya taifa letu. Nasema hivi kwa sababu zifuatazo.

1. Hajui nini taifa linataka kuelekea mageuzi ya kidemokrasia na hana uvumilivu wa mawazo ya watu wengine. Hili linadhihirishwa na matamko yake ya kutishia watumishi wa umma kuwa wale wenye mlengo wa vyama vya upinzani watashughulikiwa. Hili tamko litawafanya watawala waovu kuwanyanyasa watumishi wa umma kwa misingi ya vyama vyao na itasabibisha maafisa utumishi, wakuu wa wilaya, RC n.k kutumia mwanya huo kuwaonea watumishi wenye mawazo tofauti kwa uhai wa taifa. Wakuu wa idara za serikali ambao si waaminifu au wanaofanya ufisadi kama mabwana ardhi katika halmashauri zetu watatumia mwanya huo kujipendekeza kwa CCM, ili wale watakaotoa siri zao za ufisadi waonekane ni wapinzani.

2. Mwigulu anapaswa kufahamu kuwa CCM ndiyo yenye watumishi wa umma ambao wanafanya siasa wakati bado ni watumishi wa serikali. CCM nchi hii ina madiwani ambao ni waalimu wa shule za sekondari na bado wanafundisha na kufanya siasa. Mwigulu anza nao hao wapo halmashauri ya wilaya ya Babati vijini na mjini.

3. Mwigulu pamoja na kwamba amepitia shule hadi kuwa na shahada ya pili ya uchumi, uwezo wake wa kujenga hoja ni mdogo ndiyo maana kwenye mikutano yake anahubiri matusi badala ya sera. Sina maana kwamba Upinzania hakuna watu wabovo kama aina ya Mwigulu, hapana, wapo ila hawajafikia cheo kama cha Mwigulu. Uwezo na busara huwa ni vya kuzaliwa, shule huwa inaongezea kidogo, hivyo hataweza kuhimili vishindo vya siasa shindani. Yeye ameaanza kuhangika na personalities za watu badala ya kujenga hoja kwanini tuna umaskini na kwanini mama zetu hawana maji. Nasema hivi si kwa kumchukia Mwigulu ni kwa kumsaidia na kukisaidia chama chake na Taifa maana atasabibisha vurugu ambazo hazina maana kwa mstakabali wa taifa letu. Mwigulu mimi namfahamu, tumefanya naye siasa ya DARUSO UDSM, bwana mdogo unapya! Tatizo lake pia amelewa vyeo!

Mimi nimeamua kuyasema haya kwa sababu ninafahamu jinsi wakuu wa idara, DC, RC wanavyojua kuonea watu kwa misingi ya kuwaonea watumishi wenye mrengo wa maono kipinzani. Mimi 2000 niliandikiwa barua ya kuitwa kwa mkuu wa wilaya eti ninasadia upinzani kampeni, na kwanini nisifukuzwe utumishi. Nilimwuliza DC wewe umejuaje? Mbona nawe ni mtumishi wa umma na bado unasaidia chama chako? Nilipewa onyo na DC ambaye si mkuu wangu wa idara.
Tanzania leo hii imebadilika sana inahitaji watu wenye maono mapana ili kujenga amani.
CCM tafuteni Naibu katibu mkuu makini.

Nawatakia heri ya mwaka mpya.
 
na mimi nachukua fursa hii kumuunga mkono mtoa mada kwamba ccm inahitaji naibu katibu mkuu mwingine na si mwigulu nchemba.nimekua najiuliza ni kigezo gani kilitumika kumchagua mwigulu kushika nafasi ya unaibu katibu mkuu ccM?chama tawala chenye uzoefu wa kutosha katika medani za siasa.hivi ni kweli ccm haina watu makini kushika nyazifa kubwa kama hiyo ya unaibu katibu mkuu?kwangu mimi nimjuavyo mwigulu ana mapungufu yafuatayo:

1.hana uwezo wa kujenga hoja za msingi zaidi ya kukashifu chadema na matusi.
2.uwezo wake wa kujieleza ni mdogo sana.
3.hajui shida kubwa za watanzania kwa sasa hajui wananchi wanataka nini haswa
4.anaamini adui wa ccm ni chadema na viongozi wake
4.hajui matatizo makubwa yanayoikabili ccm kwa sasa
na hata hajui kwa nini ccm inazidi kupoteza mvuto kwa wananchi
na kwakweli ni kijana alielewa madaraka.
 
Na mimi nachukua fursa hii kumuunga mkono mtoa mada kwamba ccm inahitaji naibu katibu mkuu mwingine na si mwigulu nchemba.nimekua najiuliza ni kigezo gani kilitumika kumchagua mwigulu kushika nafasi ya unaibu katibu mkuu CCM?

C
hama tawala chenye uzoefu wa kutosha katika medani za siasa.hivi ni kweli ccm haina watu makini kushika nyazifa kubwa kama hiyo ya unaibu katibu mkuu?kwangu mimi nimjuavyo mwigulu ana mapungufu yafuatayo:

1.hana uwezo wa kujenga hoja za msingi zaidi ya kukashifu chadema na matusi.
2.uwezo wake wa kujieleza ni mdogo sana.
3.hajui shida kubwa za watanzania kwa sasa hajui wananchi wanataka nini haswa
4.anaamini adui wa ccm ni chadema na viongozi wake
5.hajui matatizo makubwa yanayoikabili ccm kwa sasa
na hata hajui kwa nini ccm inazidi kupoteza mvuto kwa wananchi
na kwakweli ni kijana alielewa madaraka.
 
hilo ni sawa na zigo la kinyes..*.
hana jipya bora hiyo nafasi angepewa hata yule mjumbe wa nec morogoro atleast jana alijaribu kujenga hoja kuliko hilo jamaa lenu akili kuambiwa ktk kipindi cha tuongee asubuhi-star tv.
Hivi haya majitu wanayaokota wapi hawa magamba?
 
Haya ni madhara ya kukurupukia siasa kwa kudhani siasa ni kusema chochote. Namshangaa huyu Mwigulu kutotambua hata misingi ya wazi ya chama chake. Amevaa bendera ya CCM lakini hajui kuwa ina alama ya JEMBE na NYUNDO vikiwa na maana ya CCM ni chama cha WAKULIMA na WAFANYAKAZI ajabu na aibu iliyoje kwa mtu mwenye wadhifa wake ndani ya chama.

Enzi za Mwalimu siasa ilikuwa ya watu wenye elimu ndogo lakini hapakuwa na viongozi wenye maneno machafu kama ilivyo wasomi wamevamia siasa na siasa imekuwa kijiwe cha wahuni wanaotukana majukwaani bila kujali wanaowasikiliza na wa rika gani na kwamba wamefuata busara na si matusi na lugha chafu.

Kwa mwendo huu tutarajie kizazi cha aina gani hapo baadaye? Binafsi nimeacha kabisa kuhudhuria mikutano ya siasa kuepuka matusi ya wanasiasa.
 
WAKUU,MTOA MADA ANA LENGO ZURI KABISA.Ila nawaunga mkono wachangiaji wanaoshauri huyu jamaa abaki na cheo chake kwani ITARAHISISHA MNO KUFIKIA MAGEUZI TUNAYOHITAJI.Maana waTZ wa leo yawezekana Nchemba hajawafahamu vizuri.Huyu dogo amelewa madaraka mno,na anachokifanya kinarahisisha mno watu kuwafahamu vizuri viongozi wapumbavu wa aina yake.KWA HIYO AACHWE AENDELEE NA NAFASI HIYO.
 
Salamu zangu za mwisho wa mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka 2013 kwa CCM ni kuhusu nafasi ya naibu katibu mkuu wake Mwigulu Chemba. CCM inahitaji kumtafuta mtu makini mwenye uwezo wa kujenga chama na kufahamu taifa linataka nini kuelekea mwaka 2015. Rafiki yangu Mwigulu ni Janga Ndani ya CCM na mstakabli wa chama chake na amani ya taifa letu. Nasema hivi kwa sababu zifuatazo.

1. Hajui nini taifa linataka kuelekea mageuzi ya kidemokrasia na hana uvumilivu wa mawazo ya watu wengine. Hili linadhihirishwa na matamko yake ya kutishia watumishi wa umma kuwa wale wenye mlengo wa vyama vya upinzani watashughulikiwa. Hili tamko litawafanya watawala waovu kuwanyanyasa watumishi wa umma kwa misingi ya vyama vyao na itasabibisha maafisa utumishi, wakuu wa wilaya, RC n.k kutumia mwanya huo kuwaonea watumishi wenye mawazo tofauti kwa uhai wa taifa. Wakuu wa idara za serikali ambao si waaminifu au wanaofanya ufisadi kama mabwana ardhi katika halmashauri zetu watatumia mwanya huo kujipendekeza kwa CCM, ili wale watakaotoa siri zao za ufisadi waonekane ni wapinzani....

Aliyemteua ndo anapenda uozo kama huo. Kwa sababu naye ni mtu wa mipasho, kwa hyo kwa akili yake fupi anadhani kumteua Mwigulu atasaidia chama kwa matusi yake. Mm naombea huyu jamaa aendelee kuwepo kwny nafasi hyo ili iturahisishie safari ya kuelekea ukombozi na uhuru wa kweli.
 
Back
Top Bottom