CCM inagawa ushindi kwa CHADEMA!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Kitendo cha CCM yangu kukamata, kushikilia na kuachia viongozi waandamizi na hata Wabunge wa CHADEMA au kuwafunga midomo wahusika hao, ni kugawa bure Majimbo na ushindi mwingine hata kabla ya 2015 kwa chama hicho kikuu cha upinzani nchini. Kiukweli, mbinu ya kutumia Jeshi la Polisi kutekeleza maagizo ya chama na Serikali hata bila ya kufikiri vyema ni kukiangamiza chama chetu cha Mapinduzi.

Amini nawaambia, viongozi wote waandamizi wa CHADEMA pamojana Wabunge wao waliowahi na wanaoendelea kupata kashkash za Polisi au Dola, wameshakabidhiwa majimbo na ushindi mwingine. Wananchi kwasasa ni wapole mno. Hawana nguvu yoyote kama silaha yao. Lakini,itakapofika 2015, mambo yatakuwa tofauti. Wananchi watakuwa wafalme kupitia kura zao. Na hawa wa kizazi hiki, hawataibiwa kura zao. 2015 ni mwaka tofauti, na uchaguzi tofauti. Dalili za kuzidi ugonjwa zitaanza 2014 kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Nakishauri chama changu kuachana na siasa chafu za kutumiaJeshi la Polisi na vyombo vingine vya Dola. Kwakuwa CCM ni chama cha siasa, ni muda sasa wa kufanya siasa. Kadiri ya uelewa wangu, siasa ni hoja za ubunifu na utekelezaji ili kupeleka mambo ya kimaendeleo mbele. Siasa si mabavu, kejeli, matusi, vitisho wala vita!

Kama chama tawala, CCM kina mambo mengi ya kufanya: kuitekeleza Ilani ya mwaka 2010-2015. Sehemu kubwa ya Ilani bado haikutekelezwa. Ilani itatekelezwaje kwa kila siku kukamata, kupiga mabomu, kushtaki na kutisha viongozi wa kisiasa NA WANANCHI KWA UJUMLA nchini? Haiwezekani, lazima CCM ibadilike. Ikinipuuza, italia na kusaga meno 2015.

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam.
 
mkuu haupo chimwaga utupakulie ya kwenye kikao chenu na wabunge?
 
Mkuu Khakha,mimi sipo Dodoma. Nilikuwa na udhuru kidogo.Lakini,ajenda kuu ni gesi asilia na nilishaarifu hilo jana Mkuu. Tupo pamoja!
 
Last edited by a moderator:
Hawaoni wala hawasikii yale tuliyokuwa tunayasikia kwa wakoloni,makaburu na tawala za kiimla kama za akina Iddi Amin sasa zimefika na kutekelezwa kwa nguvu zote na CCM ukweli mwisho wa ubaya ni ubaya haki haipokwi na wala haipotei ila inacheleweshwa
 
Hawaoni wala hawasikii yale tuliyokuwa tunayasikia kwa wakoloni,makaburu na tawala za kiimla kama za akina Iddi Amin sasa zimefika na kutekelezwa kwa nguvu zote na CCM ukweli mwisho wa ubaya ni ubaya haki haipokwi na wala haipotei ila inacheleweshwa

Dola inayo anguka hugeuka kipofu.
 
Toka lini CCM ikawa chama chako?.

Acha kudanganya watu na kuwafanya wajinga. Unaokoteza vihabari kwenye mitandao na kuanza kuunga unga kutaka kuwaaminisha wenye akili za ki-BAVICHA BAVICHA kama unafahamu lolote ndani ya CCM.

Unataka kuwaaminisha watu hata kukutana kwa wabunge wa CCM kulikuwa na ajenda ya siri.

Hilo jimbo unalofikiria kugombea kupitia CHADEMA usitegemee kama utapitishwa kuwa mgombea ubunge achilia mbali kushinda ubunge.

Kwa stories za kuunga unga kazi hizi. Thubutu!!. Bora uendelee tu na makabrasha ya uanasheria wako wa mlimani.
 
Umebugi sana mkuu Ccm haifundishwi siasa labda ujifunze kutoka ccm.
 
ccm ya sasa ni zaidi shetani...serukambi...
 
Dola inayo anguka hugeuka kipofu.

Kweli mkuu, ccm imeshakuwa kipofu kabisa. Tena kipofu ambaye ni kiziwi pia. Inaona mambo yanavyokwenda lakini kwa kuwa imeshakuwa sikio la kufa, hata utumie dawa za mitishamba haiwezi kupona.
 
endelea kujipa moyo hatuna imani tena na CCM miaka 50 ya ufukura inatosha.
 
CDM inachotakiwa kufanya ni kuhakikisha inawahamasiha vijana na makundi mengine wajiandikishe vya kutosha na wawe tayari kupiga kura mana kazi ya uenezi na campain inafanywa na itafanywa na CCM kwa sasababu ya kewweseka na CDM....Na hata sasa hivi unaona Katibu mwenezi wao akifanya mikutano au akiongea chochote anaeneza CDM
 
Jamani mmeiyona ccm? imepita hapa sasa hivi sijui inawahi wapi tena!
 
CDM inachotakiwa kufanya ni kuhakikisha inawahamasiha vijana na makundi mengine wajiandikishe vya kutosha na wawe tayari kupiga kura mana kazi ya uenezi na campain inafanywa na itafanywa na CCM kwa sasababu ya kewweseka na CDM....Na hata sasa hivi unaona Katibu mwenezi wao akifanya mikutano au akiongea chochote anaeneza CDM
 
Tatizo kubwa ni kile kitendo cha kamanda wa polisi iringa kusifiwa, na yeye bila hata kutumia chembe ndogo ya ubongo wake anakurutupuka. Kwa upande mwingine na mshukuru sana huyu kamanda kwa sababu anakipaisha cdm,ASHUKURIWE
 
Toka lini CCM ikawa chama chako?.
"-----kuwaaminisha wenye akili za ki-BAVICHA BAVICHA kama unafahamu lolote ndani ya CCM."

Unataka kuwaaminisha watu hata kukutana kwa wabunge wa CCM kulikuwa na ajenda ya siri.


Akili za KI-BAVICHA_BAVICHA ni zile zinazowashinda wana Lumumba na chama cha Magamba kuzijibu kwa hoja. Kwa maana nyingi hoja ya KI-BAVICHA_BAVICHA haijibiki kabisa na jopo la Lumumba na CCM kwa ujumla, ni hoja ya kulalamikiwa tu na jopo hilo lenye makao makuu Lumumba chini ya Nepi.

Hakuna siri ya serikali wala CCM maana zote ni dhaifu top to bottom side to side and centre.
 
CCM walikuwa wamemsahau hata MUNGU aliye hai walikuwa wamejichongea Mungu wao anayeitwa DOLA.Sasa MUNGU aliye hai ameamua kuwaonyesha ukuu wake.MUNGU aliye na historia ndefu ya kuishi hawezi kulinganishwa na DOLA hata siku moja.CCM mlijichanganya sana.Poleni sana make wote tuliwapenda lakini SHETANI Kawapenda zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…