the truecaller
JF-Expert Member
- May 8, 2019
- 809
- 940
Members JF!
Naenda kwenye mada.
Siasa za nchi hii kwa sasa zimekaa kiharakati zaidi kuliko uhalisia wake.
Kuna mambo ambayo yanaanzishwa na kukuzwa kwa kiwango ambacho kwa wafuatiliaji wa siasa za nchii hii tunauona mkakati kabambe unavyoratibiwa nchini.
Wakati mitandaoni hasa Twitter na humu JamiiForums, tunaona ID'S za wachangiaji wa kimfumo wakianzisha habari na matukio na kisha wanajipanga kuwekeana likes na comments kwa orodha ile ile na idadi ile ile.
Wakati hawa wakiwa huku,tuna lile kundi mkakati linalojumuisha baadhi ya watumishi wa taasisi za kiharakati nao wakiendeleza mapambano kwa kuichafua nchi kupitia taasisi zao kwa ushirika na baadhi ya wanasiasa wa upinzani. Baadhi wakiwa kwenye mpango rasmi na wengine kwa kutokujua wanaingizwa katika mpango ovu.
Lakini ukiingia kwa ndani unakuta engineers wa yote haya ni walioko kundi la kina membe,kwa ndoto za urais 2020 (wao wamejiapiza kwa kusema at any cost). Nachelea kusema iko siku ukweli ukidhihirika, kuna majina watanzania hataaamini kuyasikia.
Ndio maana utatu huu tunaona harakati zao kuivuruga serikali zikizidi kwa kutumia mgongo wa demokrasia.
Lengo kuu likiwa ni kuitoa serikali kwenye right track., kwamba ikose umakini wa kutimiza malengo na miradi yake kulingana na ahadi zake kwa wananchi uchaguzi wa 2015.
Na huku wale wazururaji kule wakiongeza kasi ya kuichongea tanzania kimataifa.
Kwa kuona Rais Magufuli yuko imara kuelekea uchaguzi mkuu 2020. Kuliko mwanasiasa yeyote kwa sasa.
Kwa kujua hawamuwezi kulingana na kutimiza kwake ahadi na kero za wananchi kwa asilimia 95% njia pekee waliyoiona ni hii ya sasa ya kugawana majukumu.
Wakati kundi moja likiwa linazurula nje ya nchi kutuchafua (wanasiasa wa upinzani) kwa zamu.
Kundi lingine lina ratibu mitandaoni usiku na mchana.
Kundi la tatu ni lile ambalo limejikita ndani ya chama bara na visiwani kwa vikao haramu, vyenye lengo la kumdhoofisha Rais Magufuli na serikali yake (hawa wanawatumia watumishi baadhi wa ndani ya serikali kupitia ushirika wa watumbuliwa na wahanga mbalimbali wa maamuzi ya awamu ya tano).
Lakini pia tusisahau baadhi ya wanaotumiwa ni wanaojiita viongozi wa baadhi ya madhehebu wa motandaoni.
Lengo rasmi ni kumchonganisha mheshimiwa rais na wapiga kura wake muda mfupi kabla ya uchaguzi mkuu 2020.
My take:
Kwa siasa hizi, kwa mbinu hizi, Ni wazi mnasahau kwamba mwisho wa siku waamuzi ni wananchi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania (wapiga kura).
Hata mhangaike vipi, wananchi kwa asilimia kubwa isiyo na ubishi kama si 100% basi 95% Rais Magufuli yuko mioyoni mwao na wana imani kubwa na yeye nadhani kuliko mwanasiasa yeyote kwa sasa hapa nchini.
Hivyo harakati hizi tunazoziona mkishirikiana na hao wamarekani na EU yenu.
Ni kama vile mnamuongezea umaarufu Rais Magufuli ndani ya nchi zaidi ya kumbomoa kama mnavyotaka malengo yenu yatimie.
Mnamuimarisha kwa kiasi kikubwa maana hata wazungu wakiwasaidia lakini kwenye debe la kura watanzania ndio
tutakaoamua.
#Tuko na Magufuli 2025
Sent using Jamii Forums mobile app