CCM ijisafishe iendane na kasi ya Magufuli

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
16,054
11,557
Wakati wa mchujo wa wabunge ndani ya ccm yalionekana mapungufu fulani niwakati sasa wa kuyafanyia kazi tuweze kuendana na kasi ya magufuli baadhi ya mapungufu hayo ni,

1. Daftari la wanachama lilichezewa na baadhi ya wagombea wahuni hivyo kushindwa kujua idadi halisi ya wanachama wa ccm. Ni vyema sasa itengenezwe database ili kujua idadi kamili ya wanachama wa ccm na wako wapi na wanajishughulisha na nini badala ya hili daftari kuwa mikononi mwa wajanja wachache wanaotumia mwanya wa uchaguzi kujinufaisha.

2. Udhibiti wa kadi feki, wakati wa uchaguzi baadhi ya wagombea waligawa kadi kwa makundi ya watu kwa lengo la kuwapigia kura kimsingi hawakuwa wanachama wa ccm, hivyo ipo haja ya kutengeneza kadi kwa mfumo wa smart card ambazo zitaweza kusomeka kwa kutumia mitambo maalum "card readers" ili kubaini wanachama mamluki wanaopenyezwa na wagombea wahuni.

3. Yatolewe mafunzo ya mara kwa mara kwa viongozi na wanachama ili waelewe misingi ya chama na kufahamu mwelekeo wa chama, wapo watu wanakokotwa kuelekea vyama fulani kwa mkumbo tu na hawajui malengo na itikadi ya vyama wanavyokimbilia mfano mzee wetu Mwapachu, wapo waliofanya maamuzi ya kukikomoa chama kwa kutokubaliana na maamuzi ya chama wakidhani wanakikomoa kumbe wanajikomoa wao. na mwisho wa siku wanaishia kujuta.
 
Ccm ni ileile, hawawezi kubadilika, unamkumbuka Saidi Nkumba alikuwa mbunge kule tabora, baada ya kushindwa kwenye kura za maoni ndani ya ccm alihamia chadema, chadema wanachama wa jimbo lile walipomkataa akahamia chama kingine cha upinzani, huko nako hakupata nafasi akarudi ccm, sasa usishangae akipewa ukuu wa wilaya
 
Hata kwa JIK haitakati ni ile ile jana,leo na kesho na kwanza wenyewe hawana shida ya usafi, wa nini?
 
Back
Top Bottom