CCM hatuna hoja za kumjibu Tundu Lissu, tunakwamishwa na watendaji wa Serikali

Nikupongeze kwa hoja zako zenye mizania na afya zenye kurejesha amani na imani ya wananchi.
 
Hata zisipojibiwa HAPATI KURA labda za humu kwenye mitandao ambazo hazifiki 100K.

Nyomi ya kumshangilia si hoja hata wachawi, wezi wakionekana mchana hujaza nyomi
 
Muombe Mungu akujalie akili angalau yakuweza kuchanganua Chua na mchele.
 
Nimemkote kwa mwambia angalau amuombe Mungu aweze kuchanganua Chua na mchele.

Yaani ni mburura hata kutofautisha ya kilichoandikwa na anachoongea hajui.
 
We jamaa unauelewa mkubwa sana wa propaganda.

Salute kwako mkuu. Tazama kipindi cha JK walivyoweza,kila mtu alipewa airtime yake lakini CCM kilifanya kwa ustadi mkubwa ku lainisha hoja za wapinzani.

Tukupe tu cheo cha uenezi taifa..

Serikali imefanya mengi mazuri,kwa hizo changamoto ni namna tu ya kuwaelekeza wananchi namna gani zinaenda kutatuliwa.

Sio huu upuuzi wa hao uliowataja. Wanamchafua sana Magufuli.
 
Mchuma janga hula na wa kwao....!

Baba akiwa mshamba hata watoto watakua washamba,,bandiko lako lote naona umemruka Magufuli wakati unajua kabisa huyo ndo master mind wa hayo yote.Mara nyingi tumeona akitoa kauli mbaya kwa wapinzani na za kibaguzi hadharani,amewahi pia kuwatisha wakurugenzi kuwa wasithubutu kutangaza ushindi kwa upinzani kwa kua yeye ndo anawalipa mshahara(sio serikali yaani yeye).

Mtu huyu mara kadhaa amekua na tabia ya kudhalilisha wanawake bila kusahau aliwahi kuwaambia watanzania hatuna uhuru huo na yeye ndiye ameminya uhuru wa habari,,anapenda kusifiwa ukimkosa utapewa kesi ya uhujumu uchumi au utaambiwa wewe sio raia.Mtu huyu aliwahi sema wasaliti dawa yao ni kuwaondoa masaa mawili baadae mpinzani wake kisiasa anapigwa risasi 16 na mengine mengi.Magufuli amezuia CAG asikague ofisi yake,ndege zake alizonunua(sio zetu maana hazikaguliwi),amevunja sheria na katiba yetu mara nyingi ikiwemo kujenga uwanja na kuweka mbuga za wanyama kijijini kwake pasipo kuidhinishwa na bunge.Mtu huyu aliwahi mpangia spika wa bunge eti awafukuze wapinzani bungeni ili yeye awashugulikie nje na ni kweli spika alitekeleza hilo agizo....

Ukweli huyu Mtu asafishiki hata mkijitahidi kumsafisha bila kificho ameonesha ana roho ya namna gani,kwa sasa tupo nchi yetu lakini kama tupo utumwani hatuna uhuru.
 
Kabisa na Ndo maana mpaka leo hakuna aliyejibu hoja za Lissu kiufupi hata wale wazee wanaombea CCM ianguke mikononi mwa huyu mtukufu ili wapumue.
 
NOTED MKUU na nukuu ...''' Watendaji wa serikali huu ulikuwa ndio muda wa kwenda Tbc kufanya mdahalo na watu wa upinzani kwa kuelezea mmejenga shule, Hospital na mm jifunza kitu gani na kitu gani kimebaki kwa miaka mitano ijayo sio kuelezea mafanikio tu wakati kuna mambo dhahiri hayajakamilika kwenye shule au hospital ''''

hayo uliyozungumza hiyo ndiyo polarity law . hakuna mazuri yasiyo kuwa na mafinyufinyu , wakikubali ushauri huu , ccm wameshinda asubuhi na mapema .
 
Mtoa mada kamlinda sana magu kwenye Uzi wake...😂😂😂😂 Ni watendaji tu sio rais aliyeleteleza haya Ila Ni watendaji tu. Mmeelewa watendaji😂😂😂😂😂✌️✌️✌️✌️🔥
 
Mleta Mada, hujawajua watu vizuri, hao wanaoubania Upinzani Maksudi si kwamba wanaipenda CCM ya jiwe, bali ni wapinzani wa ndani wa mlevi madaraka jiwe bin CCM. bila maadui wa ndani, adui wa nje, yaani Upinzani hawawezi kitu.

Kama kweli wewe siyo CCM kindakindaki, na unapenda Mabadiliko, usiwaamshe yaache yaendelee kuvurunda, ili kumpa Lissu kick! kwani polepole hajui kuwa anafanya kosa la ki-Siasa bana?

Kambona walimwachia huru na ulinzi juu, akaishia njia tusioijua wengi! akili unayowapa ni ya kuumaliza upinzani kinyemela! acha! Moderator fanya ujanja team Lumumba YASISOME HAPA!
 
Duh! Mkuu mbona unamwelekeza huyu jamaa kwa ukali namna hii? Inaonekana ana unazi wa kijinga?! Next time mpuuze tu nalo ni jibu pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…