Malata Junior
JF-Expert Member
- Nov 29, 2011
- 3,104
- 2,549
Kufuatia msajili wa vyama vya siasa kutangaza kufanya uhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili ya vyama vya siasa kwa upande wa Tanzania Bara,zoezi hilo linakiweka chama cha mapinduzi CCM katika hatari ya kufutwa.
Hatari hiyo ya kufutwa kwa CCM inatokana na chama hicho kukiuka baadhi ya masharti ya usajili na katiba ya chama hicho hasa katika kuchagua mwenyekiti wa Taifa ,kumiliki kikosi cha kijeshi na kufanya siasa vyuoni.
Kwa muda mrefu kumekuwepo na madai ya wanachama wengi wa CCM pamoja na wadau wa demokrasia kutaka kuwepo uchaguzi huru wa mwenyekiti wa Taifa badala ya utamaduni na desturi inayotumika hivi sasa ya kumkabidhi mwanachama aliyeshinda urais uenyekiti wa chama Taifa ambao ni kinyume na katiba ya chama hicho.
Kuhusu kumiliki jeshi ( green guard) na kufanya siasa vyuoni msajili alishawahi kuvionya vyama vyote vya siasa kusitisha mambo hayo la sivyo atavifuta lakini CCM imekaidi na bado wanaendelea nayo.
Katika barua yake ya tarehe 24 Juni 2016 msajili amevitaka vyama vyote vya siasa kutoa ushirikiano katika zoezi hilo la uhakiki litakaloanza Juni 27 mpaka Julai 6 mwaka huu wa 2016 kwani linahusu UHAI wa vyama hivyo.