Matokeo ya Urais Zanzibar na yale ya udiwani ambayo yamefanya uchaguzi wa meya kutoeleweka ni kielelezo cha CCM kutokubali kushindwa. Ni vyema sasa kama Taifa tujifunze upya maana ya demokrasia na kujiridhisha kuwa foleni za wakati wa uchaguzi zinapaswa kuheshimiwa. Kupoteza rasilimali kwa uchaguzi usiotiliwa maana ni matokeo ya taasisi dhaifu na ukiritimba wa madaraka kwa muhimili mmoja wa dola. Katiba ni suluhu la kuondoa migongano isiyo eleweka. Huko ndio tunapaswa tuanzie kwa Tanzania ya Watanzania.