CCM fanyeni haya kujitathimini

CCM fanyeni haya kujitathimini

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
57,956
Reaction score
134,037
Ni dhahiri kwamba chama hakikubaliki, haya yanathibitishwa na Magufuli kujinadi kama mgombea binafsi na kukataa kukinadi chama. Mabango yanasema ukweli, ni Chagua Magufuli tu na hakuna Chagua CCM.

Magufuli anakisema chama vibaya sana, kwamba kinalea ufisadi, kimeua viwanda nk. Pia hamna uhakika kama mgombea anakubalika au lah.

Sasa fanyeni hivi kwenye mikutano yenu

1.Msitumie malori kusomba watu toka vijijini kuja kuhudhuria mikutano,badala yake waacheni waje wenyewe kwa mapenzi yao.

2.Msilete wasanii wa Bongo fleva ibaki TOT kutumbuiza,ili muone kama watu wanafata Fid Q ama Magufuli.

3.Msiamrishe vyuo kuleta wanafunzi uwanjani,nimeona VETA,Ualimu na vyuo vyenye watoto wa boarding wakiamriwa kwenye viwanjani.

4.Waulizeni wananchi wanamtaka Magufuli au Lowassa na kwa makini msikilize idadi ya "Ndiyoooo".
 
namba 4 hapana ila yote ulosema yapo sahihi, hata mi najiuliza watafanyaje tathimin juu ya mgombea kujua anamvuto kiasi gani kwa wananchi ukiwa unatembea na lundo la wasanii, huta jua kama wananchi wanakuja kusikiliza sera za mgombea au wamekuja kusikiliza akina chege
 
Kama CCM watashindwa wajilaumu wenyewe, kelele za upinzani ni ALARM tosha ya kuwaamsha usingizini
 
Back
Top Bottom