CCM fanyeni haya kipindi cha chaguzi ndogo nitawaamini

singojr

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
5,312
6,895
Naomba wimbo wa "acha waisome namba" uendelee kutumika kwenye kampeni zenu maana hautuhusu sisi wananchi, unawahusu wapiga dili waliokula hela zetu kwa mujibu wa mwenyekiti. Uwekeni tushangilie ushindi wa kutumbuliwa kwa wapiga dili.

Msituambie tena kuwa upinzani una mafisadi maana tumekubali kukosa huduma za msingi mahakama ianzishwe na leo haina kesi. Msituambie kuwa mambo mengine yatafanyika bajeti ijayo maana tumeona bajeti iliyopitishwa bungeni sio inayotumika.

Msituambie mnajali wanyonge maana mnadeal na kununua ndege , kujenga viwanja vya ndege na kujenga daraja masaki wakati kuna watu hawana hata maji ya kunywa wala dawa.
 
Ila kura,si utatupa?
Asipowapa si huwa mnajipa wenyewe? Mwenyekiti wenu anakwapua Tsh2.7 billion za walipakodi hazina na kuwagawia Wabunge wa CCM Tsh Mill. Kumi kumi za kubrashia viatu atashindwa nini kukwapua kura?
Brushing-Leather-Shoes.jpg
 
Huwa walahi najiuliza sana kila nikiongia kitandani kulala
Mabilion haya anayotumia Rais kununua NDEGE yalipitishwa na Bunge gani?
Hapo ndipo huwa najua sisi watz WEHU tu!
 
Huwa walahi najiuliza sana kila nikiongia kitandani kulala
Mabilion haya anayotumia Rais kununua NDEGE yalipitishwa na Bunge gani?
Hapo ndipo huwa najua sisi watz WEHU tu!
Anajiamulia mwenyewe, na Dr. Tulia Ackson na Wabunge kazi yao inabaki Kumpigia mwenzao makofi.
 
Back
Top Bottom