Jee Watanganyika muliovaa Ngozi ya Tanzania hamujuwi kukutaliwa nyie? ikiwa imefika hadi Wananchi wa Zanzibar na viongozi wao na wabunge wao wa Baraza la wawakilishi wanasema basi tumechoka nyiyi bado munangagania tu hamuoni haya wala aibu nyiyi bado mumungagania tu Muungano Muungano.
Habu vunjeni Muungano sio kubweka oohh tukivunja Muungano sijuwi vitunguu vibovu na mbatata mbovu hatuwaletei oooh siju Wazanzibar waloko bara wana maduka na majumba makubwa eboo, kwani hawapo wachina na wahidi,Warundi na wengineo wenye majumba na kufanya biashara hapo na wala hawako kwenye Muungano nchi zao na Tanzania? au mumewaona wazanzibar tuu?.
Vunjeni Muungano na hao Wazanzibar walopo hapo watachagua ama kuishi hapo kwa kufuata sheria zote za nchi kama Wachina,na wengineo au watarudi Nyumbani kwao zanzibar na kupewa Good welcome kwa vile ni kwao.
Lakini sio tuze nchi yetu kwa wazanzibar eti wako Tanzania ilokuwa Tanganyika.