Ccm:chupa mpya mvinyo wa zamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm:chupa mpya mvinyo wa zamani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mtweve, Apr 11, 2011.

 1. mtweve

  mtweve Member

  #1
  Apr 11, 2011
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kilichotokea dodoma binafsi nilifahamu kitakuwa hivyo. Ndiyo! nilijua kuwa mwenyekiti kivuli wa ccm(kikwete) hana ubavu wa kuvua chama gamba ingawa sikutaka kujua ni gamba lipi linavuliwa kwa kuwa ccm ninayo ijua mimi ina magamba yasiyokuwa kuwa na idadi.Naomba nieleweke,sisemi kama mtu wakawaida,nayasema haya nikiwa kama mwanachama hai wa ccm mwenye kadi no AD 3218564. nasikitika kusema kwa mara nyingine tena ccm imeamua kuwafanyia maigizo wanachama wake na watanzania kwa ujmla. Mimi sitaki kzungumzia mkama alipo kuwa katibu wizarani,au mkurugenzi wa jiji la Dsm,mhimu kwangu ni hiki cheo chake cha mwish cha ukurugenzi wa magazeti ya serikali(TSN). Huyu ndio mkama wakati wa kampeni za uchaguzi uliopita alithubutu kuandika kwenye gazeti la daily News kuwa 'ccm itashinda Wapinzani wasitegemee" Mpaka hapa nadiriki kusema ccm wameaumua kmpa zawadi baada ya kuwasaidia kuchakachua. mhimu kwao wana uhakika wa kmwagiza lolote na asibishe kama ambavyo siku zote wamekuwa wakifanya.
  kichekesho ni kumrudisha Chiligati! kilichofanyika ni gamba tumboni wameamua kuhamishia kichwani na kufunika na nywele eti lisionekane! nakumbuka Nnape Nauye alinyamazishwa na ukuu wa wilya baada ya kuijifanya anataka kufuatilia mkataba tata wa ujenzi wa jengo la UVCCM Pale lumumba,akanyamaza leo wamempachika kwa kuwa wanauhakika wa kumnyamazisha wanatakavyo.ikumbukwe yanafanyika huku mfumo wa chama ni uleule(nalo gamba)
   
 2. H

  HomeSweetHome Member

  #2
  Apr 12, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 45
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mambo ya kiini macho haya. Hawa mabwana(CCM ) ni mabingwa wa kuwachezea mazingaombwe Watanzania. Makamba aliwahi kusema kuwa wanafahamu Watanzania ni wepesi sana kusahau mambo. Wanataka sasa kutusahaulisha uozo unaondelea kwa kuamua kufanya propaganda za 'Kujivua Gamba' hapa hamna cha kujivua gamba wala nini, CCM imeshazeeka ni mfano wa simba dume mzee, hawezi tena kufanya reproduction na kazi yake ni kusubiri simba jike shupavu aliyenawiri afanye mawindo na yeye ale hali akisubiria kifo. Ni dhahiri kuwa kwa mpango huu kifo cha CCM simba mzee kimekaribia.
   
Loading...