kibogo
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 9,739
- 4,745
Nimeshuhudia katika Taarifa ya Habari ITV ni katika kikao cha Balaza la madiwani. Madiwani wa CCM akiwemo mwenyekiti wa Halmashauri wamesema Iwapo serikali haitachukua hatua juu ya mgogolo wa Ardhi uliopo huko baina ya wananchi na wawekezaji basi wao wote watarudisha kadi za CCM na kujivua uanachama na hawataishia hapo pia watawashawishi wanachama wote wa CCM katika kata zao kurudisha kadi za CCM. Na ili kuweka msisitizo wameunda tume ya madiwani kadhaa ambao wataenda kuonana na Rais na yasipotolewa majibu sahihi wanachukua huo uamuzi mgumu.