Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 844
- 1,608
Ndoto za waliokuwa wabunge wa viti maalum mkoa wa Arusha kurejea bungeni huenda zikakwama baada ya kushindwa kuwashawishi wajumbe wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Arusha.
Wabunge hao ambao wamapata kura pungufu, sasa watasubiri huruma ya Kamati Kuu ambayo ndiyo itatoa uamuzi wa mwisho. Katika uchaguzi uliomalizika usiku wa kuamkia leo, Wanasiasa Martha Kivunge na Chiko Issa wameibuka kidedea katika kura za maoni za kusaka ubunge wa Viti Maalum (UWT) Mkoa wa Arusha baada ya kuibuka na idadi ya kura nyingi katika uchaguzi uliohusisha wagombea wengine sita.
Msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kennani Kihongosi alitangaza matokeo ya uchaguzi huo kuwa Martha alipata kura 1004, akifuatiwa na Chiko aliyepata kura 775. Wajumbe wa uchaguzi huo walikuwa 1,261.
Kura halali zilizopigwa zilikuwa 1,245 na kura saba ziliharibika.
Wagombea wengine na idadi ya kura walizopata ni pamoja na Catherine Magige (213), Asanterabi Lowassa (196), Zaytuni Swai (141), Navoi Mollel (95), Martha Amo (50) na Lilian Badi (9).