Card ya Bima ya matibabu kuna nini ?

Yukina

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2017
Posts
201
Reaction score
112
Nianza na mada yenyewe, nimekua nikitibiwa Muhimbili kwa muda sasa
Cha kushangaza ni kua Madaktari wanawadhamini sana wenye bima kuliko wakina sisi tunaolipa cash ukitokea Hospital za Wilaya hasa wagonjwa wa Public !! Udhaminiwi kabisa!! Sijui kama nitapona Mungu anajua. Huduma wanaowapa wenye bima ni tofauti na mgonjwa wa Public !! Hivi ndani ya Bima kuna nini!!??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hospital gani hiyo maana huku wengine wanawathamini wenye cash wenye bima hatuonekani umuhimu Wetu.
By the way suluhisho na wewe tafuta bima
 
Kuna siri nyuma ya pazia, kwanini Madaktari wachangamkie wenye Bima ya Afya na kuwaacha hawa walalahoi wasiokua na Bima ? Wahusika wanyeni utafiti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hospitali kwa kampuni ya bima inapata faida,mfano kidonge wewe utakacholipia kwa cash sh.10 kampuni ya bima italipa sh.100
 
daktari yeyote anayemhudumia mgonjwa wa bima ana percent kwenye matibabu ya mgonjwa huyo, mfano akihudumia wagonjwa 100 ndani ya mwezi hatachukua mshahara labda kwa matumizi ya ziada tofauti na Cash, sasa kwa nini wasikimbilie?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…