jerryempire
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 5,877
- 10,214
Ungeweka walau sample ili ieleweke, siyo wote tumeziona hizo kadi mpya.Habari,
Nikiwa kama mdau wa kuuza na kununua magari used na mapya kutoka japan imenibidi leo ni share hili jambo la card mpya zinazotolewa na TRA kwa sasa.
Kadi za mwanzo zilikuwa ni hard copy,card ambayo imetenge ezwa kwa material na kuwekwa seal maalum ambazo sisi kama (car dealer's),ilikuwa ni rahisi kugundua kama card hii ni original ama feki.
Ila mfumo wa sasa wa card hizi mpya mtu endapo kama mtu ataiiba soft copy ya card yako na ukamuazima chombo chako basi jua anaweza kwenda kukiuza pasipo wewe muhusika kujua endapo mnunuzi hatambui hatua za kufanya pindi anunuapo chombo hicho.
Japo kwa sasa tunahakiki card kupitia namba za simu za mhusika endapo majina yanaendana ya kwenye card na kwenye vitambulisho lakini hii imekuwa changamoto kwetu hasa kwa siku za weekend sababu kunawakati unakuta mtu amesajilia line ambayo haina majina yake halisi hivyo unashindwa kufanya biashara ama biashara kuhairishwa.
TRA,mnapaswa kuliangalia hili kwani card zenu mpya zinatoa mianya mingi ya watu kufanya uhalifu, uhalifu ambao mwisho wa siku huumiza watu wengi ambao wengine hawakuwa hata na hatia.
UpyaBado kama sijaelewa elewa
Siyo solution, wewe unaweza kubali mtu alipe 250k kwa ajili ya kubadili gari yako kwenda kwenye jina lake na gari yako inathamani ya 50m?Muhimu hapa, ni mnunuzi alipie baada ya kubadili jina la kadi na kusoma jina lake kwenye mfumo.
Iwe imejieleza kwenye mkataba, ni sawa na kulipia gari japani wakati gari bado hujapokea.Siyo solution, wewe unaweza kubali mtu alipe 250k kwa ajili ya kubadili gari yako kwenda kwenye jina lake na gari yako inathamani ya 50m?
Once akishachange jina gari inakuwa ya nani? Wakati huo umelipwa bei gani?
Iwe imejieleza kwenye mkataba, ni sawa na kulipia gari japani wakati gari bado hujapokea.
Pole sana mkuu mie mara kibao zinakufa unakuta card na vitambulisho vinasoma jamali lakini namba ya simu inasoma fatuma na ukimpigia simu fatuma hapokei au hapatikani so hapo uchaguzi unakuaJuzi nilikua ninauza gari almanusura biashara ife kisa hayo mambo ya kadi.
Jamaa alikua tayari kishalipa hela, kuja kucheki na mhusika mwenye jina kwenye kadi(gari ilishauzwa mara nyingi na watu walikua hawabadili umiliki)anasema hiyo gari siijui.
Mnunuzi akachukua hela yake fasta, ikabidi itumike akili na nguvu ya ziada kumrudisha kwenye mstari.