kwa kusema ukweli, adhabu ya kifo ni ya kikatili sana. wanaharakati wengi wanapigania iondoshwe. lakini mimi, nafikiri ibakie tu. kuua ni dhambi, lakini sio kuua kote ni dhambi. kuna kuua kwengine sio dhambi. ndiomaana mtu ni mtu wa mungu lakini akienda vitani kama mwanajeshi, anapiga risasi za kufa mtu kuteketeza maisha ya maadui zake. damu inamwagika na hana hatia kwake na hata kwa Mungu. kuua kunakokatazwa ni kuua bila sababu. toka zamani, mtu anayeua mwanadamu, alitakiwa auawe. hii ni haki kufanyika hivyo. kama mtu amemkata albino mikono yote miwili kama yule dana, mwenzie akafa(ile ya albino yule ni attempted murder ambayo adhabu yake ni kali vilevile). ni halali kama wakinyongwa, na kikwete asiogope kama anatenda dhambi kutia saini hawa wauaji wanyongwe hata hadharani. Mungu mwenyewe aliyemwumba mwanadamu haui, wewe usiyeumba hata unywele unamwua mwenzio, ndio maana kwetu sisi wakristo, agano la kale Mungu aliwaruhusu kuua watu kama hawa. na ilikuwa halani sio dhambi. hata kama tuko agano jipya, bado tu, anayeua anatakiwa kuuawa. atakayeua kwa upanga atauawa kwa upanga. zamani hata mchawi akikamatika alitakiwa kuuawa. kuna watu kama kina sauli kwenye bible waliwaonea huruma maadui zao ambao Mungu alimwamuru aue wote, Mungu alikasirika kwasababu hajamtii, akanyang'anya na ufalme wake. hivyo, capital punishment inatakiwa iendelee. na tunatarajia capital punishment kwa wauaji wa albino, wachuna ngozi nk. ninyi mnaopigania adhabu hii isiwepo, hamna albino kwenu,hamjawahi kuona mtu aliyechunwa ngozi na hamjawahi kuvamiwa na majambazi. usiombe yakupate ndugu, ndio utataka hiyo punishment iwepo mara mia.