Canada kusitisha ununuzi wa ndege vita za Marekani

ze kokuyo

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
7,417
9,603
Canada imeonya kwamba inaweza kusitisha ununuzi wa ndege vita za Marekani aina ya F/A-18 Super hornet kutokana na uchunguzi ulioanzishwa na kampuni ya Boeing dhidi ya kampuni yake ya utengenezaji wa ndege Bombardier.

671aaf12868d98b181e3a8709c2953a5.jpg


Dili hilo la ununuzi wa ndege 18 F18 super hornet lenye thamani ya dola bilioni mbili ($2bn) linaweza kusitishwa kwa kile kilichoitwa hatua zisizosaidia zilizoanzishwa na Boeing dhidi ya kampuni ya Bombardier.

7a5f4a7b471020fa03a5e4dfeb0bb813.jpg


Boeing inaishutumu Bombardier kwa kupokea ruzuku toka serikalini iliyoiwezesha kuuza ndege zake za abiria Cseries kwa bei chini ya ile ya soko.
422263fa9f8a220b72dfafd3bfdaf384.jpg


Uamuzi wa kuanzisha uchunguzi huo uliafikiwa na upinzani ndani ya serikali ya Canada huku waziri wa mambo ya nje wa Canada Chrystia Freeland akisema kwamba madai hayo si ya kusaidia bali ni ya kukwamisha mazungumzo ya kibiashara.

Pia Free land alieleza kwamba biashara ya anga kati ya Canada na Marekani ni jumuishi na pia inasaidia kuzalisha ajira za tabaka la kati kwa pande zote mbili.

Huku katibu wa biashara nchini Marekani Wilbur Ross akisema kwamba Marekani ni soko lililowazi zaidi duniani lakini hawatasita kuchukua hatua pale sheria zao zinapovunjwa.

Mzozano wote huu ni kutokana na Boeing kuomba uchunguzi dhidi ya Bombardier kuhusu tuhuma hizo na kuomba kuzuiwa kwa ndege hizo Cseries kufanya biashara ndani ya soko la Marekani.

Je, nini hatima ya hili?!

Na je, unazungumziaje ukuaji zaidi wa mauzo ya kijeshi kwa Marekani kwa kipindi hiki?!
f141413ee70a1e2cd4fc02f914dc68a1.jpg
b2e143d64a46f90f186e6fb223eef6ed.jpg
 
Duh! Mmarekani global arms sales share - 56.6%; Russia 8.1%. Wapi kiduku? Au zake ndio za kujilinda?
Yah... Ila ni data za 2015 labda za Urusi zitakua zimepanda kwa miaka hii miwili huwez jua
 
Nchi nyingi zimewekewa kikwazo vya kimataifa kuuza silaha zao nje mojawapo ni North Korea pamoja na Iran
 
Back
Top Bottom