CAF Champions League: Al Ahly vs Yanga 20/04/16

ESCORT 1

JF-Expert Member
Dec 7, 2015
1,368
2,890
Timu ya Al Ahly ya Misri inawaalika Yanga ya Tanzania katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika Dar Es Salaam walitoka sare ya 1-1.
Al-Ahly-vs-Yanga.jpg

Yanga ili isonge mbele inahitaji ushindi wowote ule au sare ya 2-2 na kuendelea kinyume na hapo itayaaga mashindano hayo.
-2444-b87b4.jpg

Mechi hii itaonyeshwa live na kituo cha Azam Tv kupitia chaneli yake ya ZBC two kuanzia saa 2:30 usiku kwa saa za hapa nyumbani.

Tukutane hapahapa kwenye ukumbi wetu wa JF tupeane updates kinachojiri kabla, wakati na baada ya mchezo.

Nimepata mahali hii link ya Youtube Live Stream, sijui itafaa?

===============================================================================

Updates:
Mpira ni mapumziko 0-0 bado milango ni migumu

Kipindi cha pili kimeanza

Dk 51' Hosam Ghaly anaipa Al Ahly goli la kuongoza.

Dk 55' Kipa wa Yanga Dida anaokoa shambulizi la nguvu lililofnywa na Al Ahly

Dk 60' Al Ahly bado anaongoza goli 1-0

Dk 65' Bado Yanga yupo nyuma kwa goli moja na anashambuliwa kunakotukuka.

Dk 66' Ngoma anaisawazishia Yanga goli, na matokeo ni 1-1

Dk 70' Matokeo bado ni 1-1

Dk 80' Al Ahly wanakosa goli baada ya Ghaly kuunganisha mpira wa kona na kupaisha kidogo

Mpira umesimama kwa muda kuna vurugu uwanjani baina ya wachezaji wa timu zote mbili

Dk 84' Yondani aningia badala ya Kaseke

Dk 87' Bado 1-1

Dk 88' Dida anafanya sevu ya nguvu na kuwaweka Yanga mchezoni

Dk 95' Yanga anafungwa goli la pili

Mpira Umeisha Yanga wametoka.

Al Ahly 2-1 Yanga ( 3-2 ) Aggregate
 
Timu ya Al Ahly ya Misri inawaalika Yanga ya Tanzania katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika Dar Es Salaam walitoka sare ya 1-1.
Al-Ahly-vs-Yanga.jpg

Yanga ili isonge mbele inahitaji ushindi wowote ule au sare ya 2-2 na kuendelea kinyume na hapo itayaaga mashindano hayo.
-2444-b87b4.jpg

Mechi hii itaonyeshwa live na kituo cha Azam Tv kupitia chaneli yake ya Azam two kuanzia saa 2:30 usiku kwa saa za hapa nyumbani.

Tukutane hapahapa kwenye ukumbi wetu wa JF tupeane updates kinachojiri kabla, wakati na baada ya mchezo.

cc: Makoye Matale mkolaj Katavi Amavubi

Makoye Matale kwa sasa ni Baba Askofu na amestaafu kushabikia soka
 
Makoye Matale kwa sasa ni Baba Askofu na amestaafu kushabikia soka

Wewe! Nani kakudanganya kuwa Makoye Matale kastaafu soka? Nina issues mbili zinanisumbua viz. shule na kazi hasa katika kipindi hiki cha spidi kali hata kwenye kona! Nipo sana wakuu.

Leo nitakuwepo japo matumaini ya kuwang'oa Wamisri ni madogo. Mungu ibariki Yanga Afrika, Mungu ibariki Tanzania.
 
provocations succeeded
 
Mkuu Makoye Matale, kumbe bado upo kiongozi!!!!! Aiiisee mungu akujalie kheiri umalize mission zako urudi tena humu jukwaani, I Missed you.
Ila wale members wengi wa hili kundi hasa Mikia Fans ambao ilikuwa unawafahamu siku hizi hawapatikani tena, waliobaki humu ni Amavubi, @Katavi,GENTAMYCINE.
@graffani, OKW BOBAN SUNZU, wao wako busy kumdai Hans Poppe awape timu yao.
 
Yanga imeenda kukamilisha ratiba na kutopewa adhabu za CAF kama Chad.Hongereni kwa hilo....ila hesabu za wiki zinawahusu.
Afadhali ufungwe Wiki na Waarabu kutoka Misri kuliko kufungwa kidude na Waarabu Wasukuma. Hans Poppe alisema mkiendelea kumrushia rushia mawe atamwaga bongo zenu.
 
Hakuna cha Afadhali hapo.Kama kweli nyie ni wakimataifa,vunjeni rekodi za simba.Mwenzenu kaoga 3,leo mnabugia 4.Yanga kwa marefa wabovu wa tz.
 
Kikosi kinachoanza leo Yanga;
Deo Munishi ‘Dida’,
Juma Abdul,
Mwinyi Hajji Mngwali,
Kevin Yondan,
Nadir Haroub ‘Cannavaro’,
Vincent Bossou,
Haruna Niyonzima,
Thabani Kamusoko,
Donald Ngoma,
Amissi Tambwe
Simon Msuva.
Kila la heri Yanga. Mungu ibariki Yanga. Mungu ibariki Tanzania. Amin.
 
Allah ijalie Yanga leo iwafanyie kitu mbaya Al ahly
 
Back
Top Bottom