chabuso
JF-Expert Member
- Feb 18, 2013
- 6,379
- 5,887
Nimesoma hii nakala kwenye moja ya mitandao ya jamii ya hapa tanzania, nimeona bora tunufaike sote na hii habari ya kusisimua kuhusu siasa zetu za Tanzania....
Mwandishi Maaluim
Jumatano, Agosti 16, 2017
HALI Ilivyo kwa sasa katika mgogoro wa Chama cha Wananchi (CUF), tunaweza tukasema ‘CUF bye bye’ lakini, tunapata kigugumizi kulitamka hilo kwa kuwa wananchi waliyo wengi, wanachama na viongozi wa CUF, bado wana matumaini kutokana na kesi zilizoko mahakamani.
Hakuna lisilowezekana, yumkini matarajio yao yakawa sahihi. Wapenda haki na wapenda ukweli wote wanaomba iwe hivyo, haki itendeke. CUF halisi ishinde.
Wakati huo huo, Ifahamike kuwa CUF halisi (CUF Maalim) inapambana mahakamani na mihimili miwili mikubwa . Muhimili wa serikali na taasisi zake zote na muhimili wa bunge.
Kuvuuka vihunzi hivyo, kunahitajika uadilifu mkubwa wa mahakama. Lakini pia, tujiulize kwa mfano kwamba hata CUF kife, CCM Zanzibar, ina tamaa gani kutokana na mgogoro huo?. Bado, CCM haina manusura katika hali yoyote itakayotokea!.
TUJIKUMBUSHE:
Makamu Pili wa Rais wa Zanzibar, Seif Ali Iddi katika mkutano mmoja wa hadhara wa CCM mjini Zanzibar, kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015, alisema kuwa mwisho wa CUF ni baada ya uchaguzi mkuu.
Haikuwa kauli ya mas-ghara wala utani ya kupuuzwa, ilikuwa ni kauli ya kweli iliyolenga hujuma dhidi ya CUF kwamba kisambaratike kabisa katika siasa za Tanzania na hasa Zanzibar. Yanayotokea sasa katika CUF, yanathibitisha kauli ile.
Halafu, nguvu ya Lowassa na Maalim Seif, kupitia muungano wa vyama vyao vya ‘Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) vilionekana kuwa na nguvu kubwa dhidi ya CCM, ambayo ilizidiwa sana wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu, uliyopita.
Kwa CCM haikuwa kazi rahisi kuweza kumudu nguvu na mafuriko ya UKAWA, isipokuwa kilichofanyika ni kufunika kombe. Shebaha ya CCM, mwaka 2020 wanataka kuhakikisha kuwa UKAWA wameuvuruga nyang’anyang’a, umesambaratika.
Lipumba na waliyoko nyuma yake wanafanya bidii kubwa ya kuisambaratisha CUF, tayari wameshafikia asilimia 80. Mkakati ambao lengo lake ni kuhakikisha CUF haina nguvu tena Zanzibar, ili kuiwezesha CCM, upumue.
Lipumba kwa sasa anaangazia namna ya kujiimarisha, ili kuwaonesha waliyomtuma, waliyoko nyuma yake, kwamba amefanikiwa kuweze kuisambaratisha CUF halisi, maarufu ‘CUF Maalim’. Mwelekeo wa kufanikiwa, bado ni moshi mweusi.
Alianza kutengua kujiuzulu, akaingia Buguruni, akachukuwa ruzuku ya milioni 369, kawafukuza uanachama wa CUF, wabunge wanane wa viti maalum.
Kwa mujibu wa taarifa za juu juu nilizozisikia (sijazithibitisha) kwamba anaandaa mkakati wa kuwafukuza wabunge wote wa kuchaguliwa kwa majimbo ya Tanzania Bara. Kuna kauli kwamba pia, hwenda akawafukuza na wabunge wa majimbo ya Unguja.
Inasemekana anachokifanya kwa sasa ni kuwaita, ama anawaita iwe kwa pamoja au mmoja mmoja, atakayejaribu kupingana na wito wake, ameshawaandalia mkakati. Hili litasubiri maamuzi ya kesi zilizoko mahakamani.
Inadaiwa kwamba, endapo watakaidi wito, watavuliwa uanachama na majimbo yao yatakuwa wazi, kama kawaida kazi itabaki kwa bunge na tume ya uchaguzi, kuchukuwa mkondo wake.
Bunge chini ya Spika Job Ndugai, litatafakari na kujiridhisha, kadhalika na Tume ya Uchaguzi (NEC) nayo itaitisha uchaguzi kwa majimbo hayo. Kwa ufupi, uchaguzi ya wabunge wa CUF, utarudiwa. Hatua hiyo inaweza ikakamilika ndani ya saa 48. Ni mkakati tayari uliyoandaliwa.
Akizungumza kuhusu sakata la wabunge wanane wa CUF viti maalum, Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Ramadhani Kailima alinukuliwa akisema:
“Ikiwa wabunge wa CUF watavuliwa uanachama, tume imejiandaa kwa dharura yoyote kugharamia uchaguzi mdogo.”
Kauli kama hii lazima tupigwe na butwaa kwamba, Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, anazungumzia uchaguzi mdogo kwenye majimbo ambayo bado yana wabunge wake!. Lazima tuhoji, tuseme kama si kuhujumu, ni nini?.
Serikali nzima na taasisi zake, hapa nakusudia magogoro yote ya serikali, Polisi, Msajiliwa wa Vyama, RITA, Tume ya Uchaguzi (NEC) na vingine vyote vinamtambua Lipumba.
Kuhusu kesi zilizofunguliwa kwa mgogoro huu wa CUF, ni mahakama tu ambayo wananchi bado wana imani nayo kwa asilimia japo 50. Watu hawajakata tamaa, wanaamini kuwa itatenda haki.
Bunge, ambalo lilipaswa kuwa na subira katika mgogoro wote wa CUF, kutokana na kesi zilizoko mahakamani, lakini kumbe nalo ndilo Sha’dull Minal-Qatil’, kuisambaratisha CUF.
Tukiiangalia CUF halali/CUF halisi (CUF Maalim) kama nilivyoeleza huko juu kuwa imebaki na kete yake moja tu ya mahakama baada ya makosa kufanyika huko nyuma!.
Mahakama pekee kwa sasa ndiyo imebaki kuweza kuamua kuwa CUF iwe ya nani. Mahakama ikitokea kuamua kuwa CUF iwe ya Lipumba, mtihani, ingawa si rahisi.
Tunafahamu kuwa suala la CUF, linawasononesha sana wanachama wake, wapinzani wa CCM na wananchi, bali wanajikaza na hawana budi kujikaza kwa sababu ni hujuma zinazofanywa na mihimili mikubwa ya nchi.
Makosa yaliyofanyika mwanzo kabisa kwa upande wa Maalim Seif, kumdharau Lipumba na kumuona ni mtu mmoja tu anayetapatapa kisha atatulia. Sasa yanakigarimu CUF.
Kosa hili, linatukumbusha ule msemo; ‘mdharau mwiba mguu huota tende’ hawakumuona mapema aliyekuwa nyuma ya Lipumba!.
CUF halisi, ilipuuza kauli ya Seif Ali Iddi, kuwa mwisho wa CUF ni baada ya uchaguzi mkuu. Adui wako akisema lolote, usipuuze. Waingereza wana mzemo: ‘never trust anyone’
Narudia: Huo ni wasia kwamba, usimuamini mtu yoyote katika masuala ya kazi. Maalim Seif, alikosea alipomuamini Lipumba, akiamini kuwa ataheshimu uamuzi wake wa kujiuzulu.
Lipumba ni mtwana, historia inatuonesha kuwa mtwana ana tabia sawa na mnyama. Hawezi kuwa mwaminifu katika jamii, japo jamii iwe imemuamini na kumthamini. Mwisho wa siku atadhihirisha tabia yake ya utwana.
Kupuuza kauli ya Seif Ali Iddi, pia kumpuuza Lipumba baada ya kujiuzulu na kumuachia kuendelea kuzoga kwenye ofisi za Buguruni, lilikuwa kosa kubwa, linaloitesa CUF, sasa inakaribia mwaka mmoja.
CUF, ilitakiwa kutafakari, mtu aliyejiuzulu kwa hiari yake anarudi tena ofisini usiku na mchana kufanya nini, ilhali si kiongozi?. Lipumba alikuwa tayari mwanachama wa kawaida, ilitakiwa kuwekewa mipaka anapo kwenda ofisini.
Juzi ya kinyamwezi, Maalim Seif akizungumza Vuga, Unguja alisema: “Tena walinambia hawa akina Jussa tumshughulikie asitumie ofisi…mimi ndiye niliye ruhusu.” ‘too late’
Inasikitisha, mtu mpuuzi kama Magdalena Sakaya, ambaye akiulizwa kuhusu CUF, hata hajui ilikoanzia, hajui waanzilishi wake, wala hajui malengo ya CUF, anathubutu kumpandia kichwani Maalim Seif.
Anasema, vikao vinavyofanyika Zanzibar, ni kama vikao vya ‘kitchen party’, dharau ya mwisho. Wapemba, wana msemo: ‘Hana adabu hata za kuvalia nguo’.
Hivyo, kwa mawazo na tamaa ya Magdalena Sakaya, anadhani kuwa CUF ya Lipumba, Sakaya, Nassor Seif, Habib Mnyaa, Mussa Haji, Aziza Kassim, Khalifa Suleiman na wenzao wengine kuna mtu atakayeweza kuyamini kujiunga na CUF ya wahuni.
Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa uhuru wa mwaka 1963 viongozi wa ZNP (HIZBU) walikuwa wanawatahadharisha wananchi wa Zanzibar, kuhusu kuichagua Afro Shirazi, kufanya hivyo watakuwa wameingia katika nakama na janga.
Rashid Hamad, alikuwa anawaeleza wananchi katika mikutano ya hadhara ya kampeni kwamba watakuwa wamebugi sana kuichagua ASP kwa sababu Zanzibar, itauzwa Tanganyika.
Rashid Hamad alisema: ‘Kama ni kitu cha kujaribu serikali kuwapa Afro Shirazi tungalijaribu kuwapa kwa muda wa miezi mitatu tu, mkaona cha mtema kuni’.
Kwa hivyo, tunawambia akina Maalim Seif, kama ni kitu cha kujaribu kuwapa akina Lipumba na Magdalena Sakaya na mamluki wengine, wengeondoa mahakamani kesi zote. Waachiwa CUF kwa miezi mitatu tukaona itakuwaje!.
Chini ya uongozi wa Mungiki/Lipumba, CUF kitakufa hata kabla ya mwaka 2020, kama ilivyokufa Zanzibar, chini uongozi wa ASP/CCM.
Mpaka sasa CUF ipo kama ilivyo kwa sababu ya Maalim Seif na uongozi unaomuunga mkono na mshikamano wa wananchi. Kinachosubiriwa ni uamuzi wa mahakama tu. Hapo ndiyo itajuilikana mbivu na mbichi..
Ya Mungu mengi, ikiwa akina Lipumba wameshinda mahakamani, CUF kitakuwa aina ya chama kama cha Said Soud (yeye na wake zake) hakuna mwanachama wa CUF wa kumuamini Lipumba na genge lake, wacha siku moja hata dakika moja..
Bye Bye CUF, Bye Bye CCM ya Zanzibar.. - Mzalendo.net