Busara ya Mwalimu Nyerere: Nchi haina Watu

Busara ya Mwalimu Nyerere: Nchi haina Watu

Kalamu Huru

Member
Joined
Dec 2, 2017
Posts
11
Reaction score
8
Wasalaam,

Mwalimu Nyerere alikuwa mtu mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri. Hilo halina ubishi.

Katika tafakari yake, aliandika ili nchi iendelee inahitaji mambo makuu manne (4) ambayo ni;

1. Watu
2. Ardhi
3. Siasa safi
4. Uongozi bora.

Ni wazi nchi yetu pamoja na kufanya jitihada kubwa kupata maendeleo, bado haijaendelea. Nikawaza, katika hayo manne, tunakosa lipi?

Hakika, ni wazi tunakosa WATU. Ukitafakari, Mwalimu aliposema watu hakumaanisha watu kwa idadi au uwepo. Bali ubora wa watu wenyewe pia. Mahitaji yote matatu yaliyosalia yanategemea sana ubora wa watu.

Watu bora wataweza kuitumia ardhi iliyopo kwa ufanisi na ikawa na tija. Watu bora wanaweza kuunda mfumo bora wa siasa safi. Watu bora hupelekea kuwa na uongozi bora na kupata maendeleo.

Hivyo, kama nchi, tunatakiwa kujipima na kuuunda ubora wa watu wetu.

Nani amewahi kujiuliza kwa nini Mwalimu hakutaja rasilimali fedha kama hitaji la Maendeleo??????

Kazi kwenu....!! Tunapaswa kuamua katika umoja na umojamoja wetu kujinoa kuwa bora au kubaki na uduni wenye kupelekea maendeleo hafifu na kizazi cha kulalamika kama tulivyo sasa.


0eac41bb545ff6c81ed83bd1d72dc0cc.jpg



Jamii bora hujiunda. Ikiundwa na watu wa nje, huwa ni kwa ajili ya manufaa ya watu hao wa nje.

Nawatakia majiundo mema... kama mna ujasiri wa kutaka kuwa jamii yenye maana.


The Quill.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom